Home BUSINESS TRA YAPONGEZA MCHANGO WA VYOMBO VYA HABARI KWA KUTOA ELIMU YA MLIPAKODI

TRA YAPONGEZA MCHANGO WA VYOMBO VYA HABARI KWA KUTOA ELIMU YA MLIPAKODI

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Mamlaka ya Mapato (TRA), Richard Kayombo akizungumza alipokuwa akitoa neno la ukaribisho kwa Wahariri na waandishi wa habari katika kikao kati ya Mwenyekiti wa Bodi ya TRA na Wahariri hao kilichofanyia leo Nonemba 15,2022  Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa bodi ya TRA Uledi Abbas Mussa  akizungumza na Wahariri wa habari (hawamo pichani) katika kikao na wahariri hao Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile (aliyesimama) akizungumza jambo katika Mkutano huo.

Neville Meena Mjumbe wa kamati Tendaji ya TEF akiuliza swali katika mkutano huo.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

PICHA MBALIMBALI ZA WASHIRIKI

Na: Hughes Dugilo, DSM

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukusanya mapato ya serikali jumla ya shilingi trilioni 6 katika kipindi cha mwezi Julai na Septemba mwaka huu ambayo ni sawa na asilimia 99.1 ya lengo la Mamlaka hiyo ya kukusanya Shilingi trioni 6.1.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa bodi ya TRA Uledi Abbas Mussa  katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari uliofanyika leo Novemba 15,2022 Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya shukrani kwa mlipakodi.

Amesema kuwa ushirikiano mkubwa uliopo kati ya mamlaka hiyo na vyombo vya habari katika kupeleka  elimu kwa wananchi, Mamlaka hiyo imefanikiwa kufikia malengo yake ya ukusanyaji mapato na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya habari ili elimu ya mlipakodi iweze kumfikia kila mtanzania.

“TRA imekusanya mapato ya Serikali jumla ya shilingi trilioni 6 katika kipindi cha mwezi Julai na Septemba mwaka huu ambayo ni sawa na ufanisi wa asilimia 99.1 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 6.1.”

“Makusanyo haya ni sawa na ongezeko la asilimia 14.6 ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama hicho kwa mwaka wa fedha uliopita”

“Haya ni fanikio makubwa sana kwa uongozi wa TRA katika ukusanyaji mapato ya Serikali. Hivyo nivipongeze sana vyombo vya habari kwani mmekuwa kiungo kikubwa sana kati yetu na walipakodi kwani matokeo ya makusanyo ni elimu ya mlipakodi waipatayo kutoka kwa wanahabari” amesema Bw. Uledi.

Aidha Mwenyekiti huyo wa Bodi ameongeza kwa kuwapongeza walipakodi wote kwa kujitokeza kulipa mapato ya Serikali kwa hiari yao wenyewe na kwamba kitendo hicho ni cha kizalendo.

“Kitendo cha wananchi kulipa kodi ya Serikali bila shuruti ni uzalendo wa hali ya juu sana kwani Mheshimiwa Rais Samia alishaelekeza kukusanya mapato bila shuruti” ameongeza.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amewaangiza watendaji wote wa TRA kuacha kutumia nguvu kwa walipa kodi wakati wa ukusanyaji mapato na badala yake kuangalia njia bora zaidi itakayopelekea walipakodi wenye malimbikizo kulipa madeni yao bila kuathiri shughuli zao.

Amesema kuwa Mamlaka hiyo inawaangalia walipakodi kwa macho mawili ili waendelee na shughuli zao na kuweza kulipa kodi bila tatizo lolote.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile ameishukuru TRA kwa kukutana na wahariri hao ili kupata mawazo yao na kwamba ushirikiano uliopo baina ya Mamlaka hiyo na Vyombo vya habari utasaidia kuongeza kasi ya elimu ya mlipakodi kwa wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla.

Previous articleMAJI YA KIGAMBONI YAFIKA MAGOMENI
Next articleTANZANIA MIONGONI MWA NCHI 5 UTEKELEZAJI WA KUKABILIANA NA DHARURA NA MAJANGA AFRIKA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here