Home SPORTS SIMBA YAITUNGUA IHEFU 1-0 KWA MKAPA

SIMBA YAITUNGUA IHEFU 1-0 KWA MKAPA

Timu ya wekundu wa msimbazi Simba SC imebuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu mchezo uliopigwa katika Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam. 

Simba ilipata bao la ushindi dakika ya 63 likifungwa na Pape Sakho bao lililodumu hadi dakika 90.

Kwa ushindi huo Simba imefikisha Pointi 21 nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 10 huku Azam FC wakikwea nafasi ya kwanza wakiwa na Pointi 23.

Mchezo mwingine Azam FC wameichakaza Mtibwa Sugar mabao 4_3 mchezo uliopigwa uwanja wa Manungu Mkoa Morogoro. 

Ligi hiyo itaendelea kesho katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Kagera Sugar watawakaribisha Mabingwa watetezi Yanga ambao wapo nafasi ya tatu wakiwa na Pointi 20 huku wakiwa wanacheza mechi nane.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here