Home LOCAL RAIS SAMIA AHUDHURIA MKUTANO WA 27 NCHI WANACHAMA WA MKATABA UMOJA WA...

RAIS SAMIA AHUDHURIA MKUTANO WA 27 NCHI WANACHAMA WA MKATABA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU YA TABIANCHI COP27 NCHINI MISRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi Wakuu wa nchi mbalimbali kabla ya kuanza kwa Mkutano wa kujadili mabadiliko ya Tabianchi COP27 unaofanyika katika Mji wa Sharm El Sheikh nchini Misri tarehe 07 Novemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Malawi Mhe. Lazarus Chakwera katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Sharm El Sheikh International Congress Centre.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali wanaohudhuria mkutano wa  27 wa nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya Tabianchi COP27 unaoendelea katika Mji wa Sharm El Sheikh nchini Misri tarehe 07 Novemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (kulia) mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Sharm El Sheikh kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa COP27 unaofanyika katika Mji huo nchini Misri tarehe 07 Novemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Sharm El Sheikh nchini Misri tarehe 07 Novemba, 2022. 

Previous articleDKT. KIJAJI: SERIKALI IMEKUJA NA MPANGO WA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI (MKUMBI)
Next articleRAIS SAMIA AHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA COP27, SHARM EL SHEIKH NCHINI MISRI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here