Home LOCAL PROF. NAGU AKAGUA MIRADI YA AFYA KAGERA 

PROF. NAGU AKAGUA MIRADI YA AFYA KAGERA 

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu leo amekagua miradi inayotekelezwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera na kuangalia hali ya utoaji wa huduma za afya.

Katika miradi hiyo Prof. Nagu amekagua jengo la wagonjwa wa Dharura(EMD), jengo la Mionzi na jengo la wagonjwa mahututi (ICU).

Aidha, Prof. Nagu amewapongeza watumishi wa hospitali hiyo na kuwatia moyo kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ili kuleta ufanisi katika kuwahudumia wananchi.

Prof. Nagu amefanya ziara ya siku tatu Mkoani Kagera ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya kikazi ya kuangalia utayari wa Mkoa huo katika kukabiliana na tishio la ugonjwa wa Ebola ambao kwa sasa uko nchi ya jirani ya Uganda.

Previous articleSERIKALI HAITAPUNGUZA ENEO LA HIFADHI YA MSITU WA MBIWE KWA WANANCHI – MHE.MSANJA
Next articleWAZIRI MKUU MAJALIWA AZUNGUMZA NA BALOZI WA QATAR JIJINI DAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here