Home LOCAL JERRY SILAA AAHIDI KUTOA USHIRIKIANO MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI

JERRY SILAA AAHIDI KUTOA USHIRIKIANO MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI

Mbunge wa Jimbo la Ukonga (CCM), Jerry Silaa, amesema kuwa yuko tayari kushirikiana na wabunge wenzake katika kuhakikisha tasnia ya habari inakuwa na sheria rafiki, na zinazotekelezeka.

Silaa alitoa kauli hiyo tarehe 8 Novemba 2022, wakati akizungumza na uongozi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Wadau wa Haki ya Kupata Habari (CoRI), Jijini Dodoma.

TEF na CoRI walikutana na mbunge huyo ikiwa kuzungumzia baadhi ya vipengele vilivyopo kwenye sheria ya habari yam waka 2016 vinavyokandamiza uhuru wa habari nchini.

‘‘Mimi na wabunge wenzangu tutashirikiana. Dunia imebadilika na hatuwezi kubaki hapa tulipo,’ alisema Jerry na kuongeza ‘‘nitazungumza na wenzange na kisha tutaona namna ya kufanya.’’

Kikao hicho kilichofanyika nje ya viwanja vya bunge, kiliongozwa na Deodatus Balile, Mwenyekiti wa TEF ambpo alimweleza Jerry kwamba, sheria ya habari yam waka 2016 imeweka mazingira makubwa ya kumuhofisha mwandishi wa habari.

Na kwamba, ndani ya sheria hiyo kuna vipengele mbalimbali kwa undani wake, vinaua tasnia ya habari akitolea mfano kipengele kinachompa nguvu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo kufungia chombo cha habari kwa namna anavyoona inafaa.

‘‘Katika safari ya mabadiliko haya, tumeungana taasisi zote za habari ili kuwa na kauli moja. Tumeunganisha nguvu ili kufikia lengo ’

James Marenga, Mjumbe wa CoRI kutoka Taasisi ya Vyombo ya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania alimweleza Jerry kwamba, tasnia ya habari haina tifauti na tasnia nyingine nchini katia utendaji kazi.

Marenga amabaye ni wakili wa kujitegemea alisema, ikiwa mawakili wanatengeneza taratibu zao na kuzifanya kuwa rejea katika kazi zao, inashindikanaje wanahabari nao wakajiwekea utaratibu wa ‘kujihukumu’ kama ilivyo tasnia nyingine?

‘‘Mimi ni mwanasheria, katika taasisi yetu tulitengeneza cord of conduct wenyewe na hizo ndio zinatuongozi, ni busara na wanahabari wakawa na utaratibu wao kisheria unaosimamiwa na wenyewe katika kuhakikisha maadili ya uandishi wa habari yanafuatwa,’’ alisema.

Jessy Kwayu, Mkurugenzi Mkuu wa Media Brains Inc Ltd alisema, sheria ya habari ya mwaka 2016 ilipitishwa katia mazingira ambayo si rafiki.

‘‘Vipengele 19 vya sheria hiyo vilijaribiwa kwenye sheria za nchi, vikaonekana kutoingia katika mizani ya kisheria,’’ alisema Kwayu.

Rose Reuben, Mkurugenzi Mkuu wa alisema, kwa mazingira ya sasa, waandishi wanashindwa kuandika habari kwa uhuru.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here