Home BUSINESS BRELA, ARIPO YAWAPIGA MSASA WADAU

BRELA, ARIPO YAWAPIGA MSASA WADAU

Kaimu Mkurugenzi wa Miliki Ubunifu wa BRELA Bw. Seka Kasera akizungumza kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Godfrey Nyaisa wakati alipokuwa akifungua warsha iliyohusu mifumo ya usajili kwa njia ya mtandao unaosimamiwa na Shirika la Milki Ubunifu kanda ya Afrika (ARIPO) iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Msajili Mkuu Msaidizi wa BRELA Loy Mhando akitoa mada juu ya mfumo wa Kisheria na Kitaasisi kuhusu Miliki Ubunifu katika Mkutano huo.

Mkuu wa Uchakataji maombi kutoka ARIPO , Bw. Charles Pundo (kulia) akizungumza kwa niaba ya  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Miliki Ubunifu Kanda ya Afrika (ARIPO) Bw. Bemanya Twebaze katika Warsha hiyo. (kushoto), ni Kaimu Mkurugenzi wa Milki Bunifu wa BRELA Bw. Seka Kasera.

PICHA MBALIMBALI ZA WASHIRIKI WA WARSHA HIYO

 

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), kwa kushirikiana na Shirika la Miliki Ubunifu Kanda ya Afrika (ARIPO) imetoa mafunzo kwa wadau juu ya uwasilishaji wa maombi kwa njia ya mtandao wa ARIPO.

Akifungua mafunzo hayo ya siku tatu Novemba 8, 2022 katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa, Kaimu Mkurugenzi wa Miliki Ubunifu Bw. Seka Kasera amesema mafunzo hayo kuhusu mfumo wa kisheria na wa kitaasisi wa Miliki Ubunifu yanalenga kuwawezesha washiriki na wadau ambao ni mawakala kutumia mfumo huo bila ya kupata changamoto yoyote.

“Lengo ni kuwafikia wadau ambao ni mawakala na watumiaji wa mfumo na kuwapa elimu kuhusu mfumo wa kisheria na wakitaasisi wa Miliki Ubunifu”, amefafanua Bw. Kasera.

Bw. Kasera amesema zoezi hili ni moja ya mkakati wa kuondoa na kupunguza urasimu wa uwepo wa watu wa kati (VISHOKA) wanaokwamisha taratibu za upatikanaji wa hataza kwa wafanyabishara.

Kwa upande wake Msajili Msaidizi Mkuu kutoka BRELA, Bi. Loy Mhando amesema kuwa mafunzo haya yatakuwa chachu kwa wadau ambao ni mawakala na watumiaji wa mfumo wa Miliki Ubunifu nchini, kwa kusambaza elimu hiyo kwa wananchi wengine lakini pia kupunguza kero mbalimbali na gharama za utoaji wa hataza, suala ambalo mara kwa mara Serikali imekuwa ikilipigia kelele kwa nguvu zote.

Bi. Mhando amesema mpango huu wa mafunzo umezingatia umuhimu wa wadau ambao ni mawakala kuwa karibu na wafanyabiashara, kwa kutoa huduma bora, saidizi na elimishi ili kipato chao kiongezeke na hatimaye Serikali kupata kodi na uchumi wa nchi kukua na kuimarika.

Aidha Mkuu wa Uchakataji maombi kutoka ARIPO Harare, Zimbabwe, Bw. Charles Pundo akiwasilisha mada kuhusu taratibu na hatua za kusajili Alama za Biashara na Huduma kupitia mfumo wa ARIPO, ametoa rai kwa BRELA na wadau kujitokeza kwa wingi ili kutumia vyema fursa ya kuomba maombi mapya kwa njia ya mtandao.

Mafunzo haya yanatarajia kufikia tamati Novemba 10, 2022.

Previous articleMUUNDO MPYA IDARA YA TIBA KURAHISISHA UTOAJI HUDUMA KWA KWA WAZEE
Next articleJERRY SILAA AAHIDI KUTOA USHIRIKIANO MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here