Home BUSINESS EMIRATES YAADHIMISHA MIAKA 25 YA HUDUMA ZAKE NCHINI TANZANIA

EMIRATES YAADHIMISHA MIAKA 25 YA HUDUMA ZAKE NCHINI TANZANIA

Na: Mwandishi wetu

KAMPUNI ya Ndege ya Emirates inaadhimisha miaka 25 ya huduma nchini Tanzania, 

kusaidia kuunganisha abiria na wafanyabiashara kutoka Dar es Salaam na duniani kote huku ikitaja mafanikio yake makubwa ya kukua kishughuli zake nchini.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mwishoni mwa wiki hii na Meneja wa Nchi wa Emirates nchini Tanzania,Abdullah Adnan alisema tangu mwaka 1997, Emirates imejivunia kuunganisha karibu wasafiri milioni 3 kwa zaidi ya safari 15,000 za ndege kati ya Tanzania hadi Dubai .

Alisema shirika lao la ndege limezidi kukua kishughuli nchini na kufanya kuwepo kuanza kwa  safari za  ndege mara moja kwa wiki inayoendeshwa na A310-300, kati ya Dubai na Dar Es Salaam.”Huduma za shirika hili letu zinazidi kukua  na kufikia hadi safari za kila siku zinazohudumiwa na shirika la ndege la Boeing 777-300ER, kulingana na mahitaji ya abiria na mizigo,”Ilisema sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza.

“Miaka miwili iliyopita imekuwa migumu kwa watu wengi na viwanda, lakini Kampuni hiyo ya  Emirates imekuwa  ikifanya kazi kwa bidii ili kujenga upya mtandao wake kwa usalama huku ikiweka kipaumbele kwa wateja wake, wafanyakazi, na jumuiya inazohudumia duniani kote,”Alisema.

Alisema walipaa  angani na kufika Tanzania kwa mara ya kwanza miaka 25 iliyopita, wakiwa na dhamira  ya kuunganisha wasafiri wa Tanzania na duniani kote, na kuwapa uzoefu ambao uliendana na  mahitaji yao,.

“Tunajivunia hatua hii muhimu,  na tuna heshima kubwa kuitumikia Tanzania kusaidia kuleta familia pamoja, kusafirisha watalii kwa ndege katika nchi hii nzuri na kuonyesha vivutio vyake, na kusaidia kuongeza nguvu za uchumi wake,” alisema na kuongeza 

“Tunajivunia kwamba tumeweza kuimarisha uchumi kupitia shughuli zetu za SkyCargo, na  tunapanga kuendeleza dhamira yetu ya kutumikia Tanzania kupitia uzoefu wa hali ya juu wa  usafiri wa anga na kwa kusaidia jamii na uchumi wa ndani,” aliendelea.

Alisema Emirates SkyCargo imekuwa ikisaidia uchumi wa Tanzania kwa kuwezesha mauzo ya nje 

kwenda duniani kote. Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, Emirates SkyCargo, imebeba zaidi 

ya tani 660,000 kwenda na kurudi Tanzania. Mizigo ya nje ya Dar Es Salaam mara kwa mara 

inajumuisha vitu vinavyohitaji uhifadhi wa makini kama vile nyama ya mbuzi na kondoo, 

samaki kaa, kamba na parachichi. SkyCargo pia inasaidia kuagiza sehemu za mashine pamoja na 

vifaa vya elektroniki nchini. Emirates SkyCargo pia ilikuwa nguzo ya nguvu kwa jamii ya wenyeji wakati wa janga la kiafya kwa kusafirisha na kutoa vifaa muhimu vya matibabu na chanjo.

Previous articleJERRY SILAA AAHIDI KUTOA USHIRIKIANO MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI
Next articleTUJIPANGE KWA MAFUNZO, VIFAA KUKABILIANA NA MAJANGA YA AJALI MBALIMBALI 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here