Home LOCAL JARIDA LENYE TAARIFA SAHIHI ZA KISAYANSI KUZUIA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA LAZINDULIWA DSM

JARIDA LENYE TAARIFA SAHIHI ZA KISAYANSI KUZUIA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA LAZINDULIWA DSM

Na: Hughes Dugilo
Kampuni ya Baobab Shalom imezindua Jarida la Sayansi litakalo wawezesha watoto kupata taarifa sahihi za kisayansi na kujua namna ya kuzuia magonjwa yanayoambukiza duniani.

Jarida hilo la kisayansi liitwalo “OYLA Africa Magazine” limezinduliwa jijini Dar es Salaam Leo kwa lengo la kuwawezesha watoto kuwa na uwezo wa kuchunguza, kukusanya taarifa na kuzikabili changamoto za dunia iliyopo nje ya shule.

Akizungumza wakati wa uzinduzi Meneja wa OYLA Africa Godfrey Lugalambi amesema jarida litamuaanda mtoto na mzazi nje ya maisha ya shule aweze kuongeza ujuzi katika kukusanya taarifa, na kutafiti majibu sahihi ambapo itawezesha kufanya maamuzi binafsi pevu na yenye uhuru.

“Hii ni jarida bora kabisa na la kwanza la kisayansi kwa Tanzania na Africa yote. Ni chapisho la kila mwezi maalum kwa wanafunzi na wazazi ambapo limesheheni uchambuzi wa kisayansi, hisabati, fizikia na Tehama,” ameeleza.

Ameeleza kuwa wameamua kwa makusudi kuchapisha Jarida hilo kwa njia ya karatasi, ili kumrahisishia msomaji asilazimike kutumia intaneti au vifaa vya aina nyingine kupata taarifa japo huu ni ulimwengu wa digitali.

Mkurugenzi OYLA Africa Yevgemiy Semikov amesema jarida hili linaweza kusomwa na familia nzima, kuazimwa na marafiki na kutolewa kama zawadi kwa maktaba za shule. Jitihada zetu zinalenga kumwongezea mtoto maarifa na pia kuhakikisha inafikia walengwa wote sio shule tu za mjini lakini hata za vijijini.

“Tunatoa wito kwa wadau kuunga mkono jitihada hizo ikiwemo kupata nakala jarida hilo na kuendelea kushirikiana pamoja katika kuhakikisha linaboreshwa kwa ajili ya kuandaa kizazi kilicho bora kinachoweza kupambana na mazingira yanayowazunguka,” ameeleza.

Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Alhaji Abdul Maulid amesema elimu ni gharama, Serikali inaposema inatoa elimu Bure haimaanishi kuwa ni Bure, inagharamia vitabu, mishahara, hivyo wazazi wachangie kununua vitabu kwa ajili ya watoto wao watakavyosoma wakiwa shuleni na nje ya mazingira ya Shule.

“Gazeti hilo litasaidia watoto wanajijengea utamaduni wa kusoma, likisomwa lakini pia wanakuwa na dhana ya Utafiti na ya kisayansi,” amesema.

Nae Mwakilishi kutoka Shule ya Sekondari Tusiime Jenipher Kaizilege amesema Jarida hilo la kisayansi limeandaliwa vema, limerahisisha vitu vingi na kuweka katika njia ya picha na michoro ambapo itamvutia mwanafunzi kusoma na kuelewa kwa haraka, nadharia imepeleka kwenye vitendo.

“Mwanafunzi ataitumia muda wake mwingi kulisoma badala ya kupekua simu janja ambapo analazimika kuona na mambo mengine yasiyofaa, pia litakuwa ni dhana ya kufundishia kwetu sisi walimu wa Sayansi kwa kuwa limesheheni vitu vingi sana,” ameongeza Kaizilege.

Previous articleTFC YAELEZA MIKAKATI YAKE KWENYE WIKI YA HUDUMA ZA KIFEDHA JIJI MWANZA
Next article ZIARA YA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN WILAYANI MONDULI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here