Home BUSINESS DKT. KIJAJI: SERIKALI IMEKUJA NA MPANGO WA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA...

DKT. KIJAJI: SERIKALI IMEKUJA NA MPANGO WA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI (MKUMBI)

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na Wahariri, na waandishi wa habari (hawamo pichani), alipokuwa akifungua mafunzo ya  Wahariri na Waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya utelekezaji wa mipango wa kuboresha Biashara ya uwekezaji.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Ali Gugu akizungumza alipokuwa akitoa neno la utangulizi na kumkaribisha Mgeni rasmi kuzungumza katika Kikao hicho.

Sehemu ya waandishi na Wahariri wa habari wakiwa kwenye kikao hicho 

Picha ya pamoja

Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa Kufuatia mpango wa  ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara na Uwekezaji nchini imeweka mazingira rafiki kwa wawekezaji ili kuwafanya waweze kuwekeza kwenye sekta mbalimbali za kiuchumi.

Hayo yameyasema Jijini Dar es salam Novemba 6,2022 wakati akifungua  mafunzo ya  Wahariri na Waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya utelekezaji wa mipango ya kuboresha Biashara ya uwekezaji.

Waziri Kijaji amesema kuwa serikali kupitia Wizara hiyo imekutana na  watu wa Sekta Binafsi wenye viwanda na kuwaelekeza kuainisha changamoto zao ili zipatiwe ufumbuzi ambapo ameongeza kuwa kuanzia mwezi wa Disemba mwaka huu serikali inakusudia kuanzisha mchakato wa kubadilisha sheria  zinahusu masuala ya kodi.

“Serikali ya awamu ya Sita(6) imeamua kufungua milango ya majadiliano na wawekezaji wa sekta binafsi  kwa ajili kuzungumza, kujadiliana ili kupata  majawabu mazuri kati ya serikali na sekta binafsi”amesema Waziri Kijaji.

Aidha  Dkt. Kijaji ametoa rai kwa Wahariri na Waandishi wa habari kushirikiana  na wizara hiyo katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya mpango huo na kwamba kwa kufanya hivyo kutaongeza chachu kwa wawekezaji  na wadau mbalimbali kujitokeza kwa kufanya uwekezaji na Biashara kwa ujumla.

 Aidha amesema kuwa  baadhi ya sheria zilizotugwa au kufanyiwa marekebisho ni pamoja na masuala ya usuluhishi wa migogoro ambapo serikali imefuta kipengele (16)2 cha sheria ya makampuni ili kuondoa takwa la kugongewa muhuri na kamishina wa viapo, pamoja na marekebisho ya  kifungu cha 60 cha sheria ya ushindani kinachohusu adhabu ya makosa ya ushindani ili ihusishe pato ghafi lililopatikana ndani ya Tanzania Bara na si Duniani kote.

Hata hivyo amebainisha kuwa serikali imefanya mabadiliko ya sheria na kanuni mbali mbali kuondoa muingiliano wa majukumu ya Taasisi na mamlaka za udhibiti, miongoni wa muingiliano ulioondolewa ni pamoja na jukumu la kusimamia usalama wa chakula na vipodozi kutoka iliyokuwa mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) kwenda shirika la viwango Tanzania (TBS).

Waziri kijaji ameongeza kuwa Utekelezaji wa mpango wa kuboresha Biasharana na Uwekezaji (MKUMBI) unafuata misingi na utendaji kazi, huku akitaja misingi inayopaswa kuzingatiwa katika utekelezaji wa  (MKUMBI) ambayo ni pamoja na Maboresho yanayofanywa na mamlaka husika yasilenge kuongeza mapato bali kukidhi gharama za utoaji huduma  ,ukusanyaji wa mapato kutumia nyenzo rahisi na rafiki kwa kuweka vituo vya pamoja vya huduma au kuunganisha mifuko.

Misingi mingine ni kuondoa mwingiliano wa majukumu ya Taasisi kwa kuunganisha majukumu ambayo yanaingiliana

sheria, kanuni na taratibu zilenge kutekeleza sera za Biashara ushindani  kumlinda mlaji na huduma za uma ,Udhibiti uwe wa kuendeleza sekta husika au uzalishaji ili kukuza ushindani wa kimkakati wenye usawa, tija na Ubunifu kwa kupunguza tozo na ada,kuwa na mifumo ya udhibiti yenye uhakika endelevu na inayotabirika.

Pamoja na kanuni zote zitakazotugwa zifanyiwe tathimini ya adhari ya uthibiti kabla kuidhinishwa kutumika kuhakikisha kuwa maboresho ya kupunguza kanuni hayaondoi mamlaka uthibiti kutatua changamoto za kiutendaji ndani na baina ya mamlaka za uthibiti.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here