Home BUSINESS BRELA YAPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA KWENYE MKUTANO MKUU WA 46 WA ARIPO

BRELA YAPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA KWENYE MKUTANO MKUU WA 46 WA ARIPO

Tanzania inashiriki katika Mkutano wa 46 wa Baraza la Uongozi la Shirika la Miliki Ubunifu Kanda ya Afrika (ARIPO), kujadili taarifa mbalimbali za utendaji kazi wa ARIPO na kupitia taarifa mbalimbali za Itifaki zinazosimamiwa na ARIPO

Mkutano huo ulioanza leo leo tarehe 21 Novemba, 2022 Maputo, Msumbiji, unahudhuriwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa, Afisa, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA), Bi. Mariam Jecha Kaimu Mkurugenzi wa Miliki Ubunifu Bw. Seka Kasera pamoja na mwakilishi kutoka ofisi ya Hakimiliki Tanzania Bw. Philimon Kilaka.

BRELA kama Ofisi ya MIliki Ubunifu nchini imekuwa mshiriki mkubwa wa ARIPO kwenye masuala mbalimbali yanayohusu Miliki Ubunifu kwenye Ukanda wa Afrika. Katika Mkutano huo masuala mbalimbali yatajadiliwa hasa kuhusu Hataza, Maumbo Bunifu, Alama za Biashara na Huduma, Hakimiliki na linzi zingine za Miliki Ubunifu.

Wadau mbalimbali wa ARIPO ikiwa ni pamoja na Mashirika ya Kimataifa na Kikanda wameshiriki kwenye ufunguzi wa mkutano. Kwa upande wa Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) limewakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa WIPO Bw. Daren Tang.

Mkutano huo wa siku tano utakaohitimishwa tarehe 25 Novemba, 2022 umefunguliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Msumbiji, Mhe. Silvino Mareno.

Nchi wanachama 22 wa ARIPO zinashiriki ikiwa ni pamoja na WIPO na mashirika mengine ya kikanda na kimataifa.

Previous articleKATIBU TAWALA MKOA WA MWANZA ATEMBELEA BANDA LA BoT KWENYE MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA
Next articleWAZIRI NAPE: SERIKALI IMEPOKEA MAONI YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here