Home LOCAL AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI GEITA

AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI GEITA

Mtu mmoja alietambulika kwa jian la Amin Salum anaekadiliwa kuwa na umri kati ya miaka (25-29) Bodaboda ameuwawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi Katika mtaa wa Nyamalembo wilaya ya Geita Mkoani Geita.

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Geita Kamishina Msaidizi wa polisi (ACP) Safia Shomary amethibitisha kutokea kwa tukio hilo amesema chanzo cha mauaji hayo ni majambazi walikua wanataka kumpora mfanya biashara mmoja ambae jina lake limehifadhiwa mara baada ya kuwakimbia majambazi hao akitaka kusaidia na madereva Bodaboda katika eneo la Nyamalembo wilayani Geita.

Kamanda Safia amesema baada ya mhanga wa tukio kupata msaada kutoka kwa bodaboda ndipo wakaanza kuwafukuza majambazi hao hali iliyopelekea majambazi hao kumfyatulia lisasi Amin Salum na kusababisha kifo chake.

Jeshi la polisi Mkoa wa Geita linaendesha msako mkali kwa lengo la kuhakikisha wale wote waliohusika katika tukio hilo la mauaji wanakamatwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here