Home SPORTS YANGA YAENDELEZA UBABE WA SHINDI, YAILAZA KMC 1-0 KWA MKAPA

YANGA YAENDELEZA UBABE WA SHINDI, YAILAZA KMC 1-0 KWA MKAPA

MABINGWA Watetezi Yanga leo wameendeleza vyema katika kutetea taji lao la ubingwa Kwa msimu huu baada ya kuichapa KMC bao 1-0 katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo uliokuwa na ushindani kwa timu zote mbili mpaka kufika mapumzika hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la npinzani wake.

Katika dakika ya 80 mshambuliaji wa timu hiyo Feisal Salum aliipatia Yanga bao la pekee ambalo limeipatia Yanga alama 3 pekee na kushika nafasi ya kwaza katika msimamo wa ligi.

Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 17 katika mchezo wa saba na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu, ikifuatiwa na Mtibwa Sugar yenye pointi 15 za mechi tisa na Simba pointi 14 za mechi sita.

KMC baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake 13 za mechi tisa nafasi ya sita.

Previous articleWAZIRI UMMY AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA SHIRIKA LA IDADI YA WATU DUNIANI NCHINI TANZANIA
Next articleDAWASA YATOA RATIBA YA MGAO WA MAJI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here