Home BUSINESS TRA GEITA YATOA ELIMU YA KODI KWA WAFANYABIASHARA NYANG’HWALE

TRA GEITA YATOA ELIMU YA KODI KWA WAFANYABIASHARA NYANG’HWALE

Afisa elimu na huduma kwa mlipa kodi TRA Mkoa wa Geita Justine Katiti akizungumza na wafanyabishara wa wilaya ya  Nyang’hwale Mkoani humo.

Baadhi ya Wafanyabishara wakimsikiliza Afisa huyo wa TRA Wilayani Nyang’hwale

 Na: Costantine James, Geita.

Wafanyabiashara wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita wametakiwa kusajili na kurasimisha biashara zao kwa lengo la kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) hali itakayowasaidia kukidhi vigezo vya kupata tenda mbalimbali katika makampuni ndani na nje ya Mkoa wa Geita.

Rai hiyo imetolewa na ofisa elimu na huduma kwa mlipa kodi kutoka Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Geita Justine Katiti wakati akizungumza na , wafanyabishara hao Busolwa na Kharumwa wilayani Nyang’hwale.

Katiti amesema wafanyabiashara wanapaswa kuwa na kasumba ya kuweka kumbukumbu za biashara zao ili kuwawezesha kupata fursa mbalimbali ikiwemo kupata fursa ya kukopesheka kwenye taasisi za kifedha pindi wanapokuwa na taarofa zao sahihi za biashara zao.

Amesema katika kutunza kumbukumbu sahihi za biashara wanazozifanya wafanyabiashara hao wanapaswa kutumia mashine za Kielektroniki za Risiti (EFD) kwa lengo kuepuka kufanya makadirio yasiyo sahihi na yenye udanganyifu katika biashara zao.

Nao baadhi ya wafanyabiashara wilayani Nyang’hwale wameipongeza mamlaka ya mapato nchini (TRA) Mkoa wa Geita kwa kuwapatia elimu itakayowasidia katika kuongeza ufanisi na uwajibikaji katika biashara zao kwa lengo la kuongea ukusanyaji wa mapato hali itakayosaidia serikali kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato.

Previous articleRAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHUTUBIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA SHIRIKA LA WANANWAKE KATIKA SHERIA NA MAENDELEO BARANI AFRIKA (WildDAF) JIJINI DAR ES SALAAM
Next articleWAZIRI GWAJIMA ATOA CHETI KWA MWENYEKITI  MALAGASHIMBA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here