Home LOCAL TAMASHA LA JINSIA KANDA YA KASKAZINI LAFUNGWA SAME..DC MPOGOLO ATAKA SHERIA ZITUMIKE...

TAMASHA LA JINSIA KANDA YA KASKAZINI LAFUNGWA SAME..DC MPOGOLO ATAKA SHERIA ZITUMIKE KUMALIZA UKATILI WA KIJINSIA

Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo akifunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini.
Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo akizungumza wakati akifunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo amefunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro huku akihimiza kila mmoja kuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kusisitiza Mila na desturi ziendelee kuwepo lakini sheria itawale.
 
Mpogolo amesema Dhamira ya serikali ni kuhakikisha mila na desturi kandamizi zinafutwa hivyo ni wajibu wa kila mwanachi anakuwa mstari wa mbele kutokomeza ukatili wa kijinsia.
 
“Mila na desturi ziwepo lakini sheria itawale, ukiacha mila na desturi zitawale lazima kuna kundi la watu litakandamizwa. Kuna watu wanatumia mila na desturi kuharibu sheria hivyo kuathiri sheria kuchukua mkondo wake. Hongereni sana TGNP Warsha hizi, matamasha haya yanasaidia sana huku pembezoni”,amesema Mpogolo.
 
“Nawaahidi serikali itakwenda kusimamia yale yote tuliyokubaliana kwenye tamasha la jinsia ikiwemo kutokomeza mila kandamizi. Changamoto kubwa ni mila na sheria zetu, hakuna mtu yeyote atakayeweza bila sisi wenyewe kuamua kuziweka pembeni mila kandamizi zinamkandamiza mwanamke”,ameongeza.
Mkuu wa wilaya ya Same Mhe. Edward Mpogolo akisalimiana na washiriki wa Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini.
 
Aidha amewahamasisha wanawake kujitokeza kugombea nafasi za uongozi kuanzia ngazi ya serikali za mitaa na kuingia kwenye vyombo vya maamuzi.
 
“Kina mama mna nguvu, sasa hivi hakuna mama wa nyumbani Mama zangu , dada zangu tunaishi kule mtaani tuna nafasi ya kugombea kwenye serikali za mitaaa, kule ndiko kaya zinakopatikana na ndiko kuna vyanzo vya ukandamizaji. Huko ndiko wajane waliko, huku kwenye ofisi zetu wanaokuja ofisini ni wajane wanalalamika ardhi zao kudhulumiwa. Haki ya umiliki wa ardhi imekuwa changamoto kwa wajane, watoto wa kike hawapewi haki lazima haya tuyaondoe”,amesema Mpogolo.
 
“Nilichokiona ni namna gani TGNP ina ushirikiano na wadau mbalimbali, mmealika wageni kutoka ngazi ya kitongoji hadi mkoa. Tunawahakikishia wanawake kuwa nafasi za kuingia vyombo vya maamuzi lakini msikengeuke, kuna baadhi wakiingia huko wanakengeuka, msimamie vizuri ili kulinda haki za wanawake, msitumie msumeno kukata vibaya mnapoingia kwenye vyombo vya maamuzi”,amesema.
Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo.
 
Mpogolo ameipongeza TGNP na wadau wake kwa kulifanikisha Tamasha hili la kanda ya Kaskazini ambapo washiriki wamepata fursa ya kujadili kwa kina, na kubadilishana uzoefu kupitia mada mbalimbali zilizofanyika katika jopo na warsha mbalimbali ambazo zilijikita katika kuangalia masuala ya fursa za kilimo, uimarishaji wa huduma za kijamii, uongozi shirikishi na mila kandamizi. Mada zote hizi ziliongozwa na mada kuu ya Tamasha hili Jinsia isemayo, “Haki za Kiuchumi:Rasilimali ziwanufaishe wananchi waliopo pembezoni kwa Maisha endelevu”.
 
“Nimearifiwa pia mijadala hiyo ilitoa mapendekezo na maazimio mbalimbali yenye mrengo wa kusaidia Serikali na Halmashauri ya Wilaya ya Same katika kutekeleza na kusimamia masuala nyeti ili kufikia Haki za Kiuchumi hususan kwa makundi yaliyo pembezoni, pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazokwamisha ufikiwaji wa fursa kwa makundi hayo”,amesema Mpogolo.
 
“Nimefarijika zaidi baada ya kuarifiwa ya kwamba washiriki wote waliofika hapa, zaidi ya 500 wameweka azma ya kwamba kila mmoja kuwafikia angalau wanajamii watano (5) na kuwahamasisha kujiunga kwenye harakati za kuwainua wanawake na makundi ya pembezoni katika kutambua, kufikia na kutumia fursa za kiuchumi ili kuleta maendeleo katika ngazi ya kaya, Kijiji, Halmashauri na hatimaye kitaifa. Huu ndio unapaswa kuwa msingi wa kujenga uchumi wetu na kudumisha mshikamano baina ya makundi mbalimbali kwenye jamii. Huu ndio Uzalendo na ndio njia sahihi inayostahiki kuunga mkono jitihada za Serrikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika kufika usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu”,amesema Mpogolo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi.
 
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi ameyataja baadhi ya maazimio yaliyofikiwa kwenye Tamasha hilo ni pamoja na Wajumbe wa Kamati za Vijiji kuweka hamasa na kutumia fursa mbalimbali za kujiongezea uwezo na uelewa kuhusu elimu ya afya ya uzazi ili kuwa mstari wa mbale katika kusimamia kwa ufanisi wa utoaji huduma hizo.
 
“Maazimio mengine ni Serikali za Vijiji kwa kupitia Utaratibu uliowekwa na TAMISEMI wa Fursa na Vikwazo vya Maendeleo (yaani O&0D) kutambua na kuweka kuwa kipaumbele upatikanaji wa vifaa tiba na idadi ya kutosha ya watoa huduma kwenye zahanati na vituo vya afya na Kuchagiza mapitio na marekebisho ya sheria (Uchaguzi Serikali za Mitaa) na Kanuni ili kuweka mazingira wezeshi kwa wanawake na makundi mengine kujumuishwa na kushiriki kikamilifu kugombea nafasi za uongozi na vyombo va maamuzi katika ngazi mbalimbali”,amesema Liundi.
 
“Pia Kuboresha mfumo na utaratibu wa utoaji wa mikopo ya Halmashauri na mafunzo ya uendeshaji miradi/biashara na utunzaji wa fedha kwa wanawake, vijana na makundi mengine ili kupunguza urasimu na kuwezesha upatikanaji rahisi wa taarifa kuhusu fursa kwa makundi hayo na Kuhamasisha vikundi vya kijamii (wanawake, wanaume, vijana, wazee, watu wenye ulemavu) na Viongozi wa mila na dini ili kuwa mstari wa mbele kutoa elimu na kuongeza uelewa kwenye jamii kuhusu haki za wajane kurithi na kukemea ukatili na dhuluma za ndoa za utotoni na ukeketaji”,ameongeza.
 
Maazimio mengine ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya, hususani, maafisa biashara kwa kushirikiana na sekta binafsi na taasisi zisizo za kiserikali kuwapatia taarifa (kupitia teknolojia ya simu) na kuwajengea uwezo wanawake na makundi mengine ya pembezoni wanaoshiriki katika kilimo kutambua na kufikia masoko na kunufaika na bei nzuri kwa mazao yao.
 
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali amesema sheria ndiyo msumari wa kumaliza matukio ya ukatili huku akihamasisha wanawake wasiachwe nyuma kwenye masuala ya maendeleo.
 
Mwakilishi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Makundi Maalum, Bi. Bahati Majwala amewahamasisha kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa kwenye halmashauri, kwenye wizara, benki ya biashara Tanzania akibainisha kuwa Serikali inaendelea kuwajengea uwezo wanawake wajasiriamali kuhusu elimu ya vifungashio na namna ya kuandaa bidhaa na kuhamasisha wanawake kujiunga kwenye vikundi.
 
Naye Mratibu wa Jinsia OR-TAMISEMI, Linus Kahendaguze amesema Mikopo inayotolewa na halmashauri imeboreshwa sasa inafanyika kidigitali na imeendelea kuwanufaisha wananchi na serikali imeendelea kutoa fedha nyingi mfano Mwaka 2021 ilitoa shilingi Bilioni 62 ambapo asilimia kubwa ya wanufaika ni wanawake.
 
“Rais Samia ni kinara wa masuala ya kijinsia ndiyo maana ameendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wanawake ikiwemo fursa za mikopo,kilimo. Ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kila anazuia ukatili wa kijinsia. Tunatakiwa kuishi katika mazingira ya amani, tutoea taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia”,amesema.
 
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo akizungumza wakati akifunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo akizungumza wakati akifunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi  akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi  akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro

Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro

Rose Ngunangwa akiwasilisha taarifa ya mambo yaliyojiri kwa niaba ya TGNP wakati wa Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro
Mratibu wa Jinsia OR-TAMISEMI, Linus Kahendaguze akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) 
Mwakilishi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Makundi Maalum, Bi. Bahati Majwala akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) 
Mratibu wa Kituo cha Maendeleo ya Watoto na Vijana KKKT Dayosisi ya Pare na Compassion Tanzania akizungumza kwa niaba ya washiriki wa Tamasha wakati wa kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Annastazia Tutuba akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) 
Hafla ya kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini ikiendelea

Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo akiagana na washiriki wa Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same

Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Edward Mpogolo akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali (kushoto) baada ya kufunga Tamasha la Jinsia Kanda ya Kaskazini leo Ijumaa Oktoba 7,2022 lililofanyika kwa muda wa siku tatu (Oktoba 5-7,2022) katika viwanja vya Kwasa Kwasa Wilaya ya Same.
 
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
[10/7, 4:32 PM] +255 688 405 951:

Previous articleNSSF YAWAHIMIZA WACHIMBAJI WADOGO, WAJASIRIAMALI KUJIUNGA NA MFUKO HUO.
Next articleMBIBO AUNGA MKONO JUHUDI ZA STAMICO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here