Home BUSINESS NSSF YAWAHIMIZA WACHIMBAJI WADOGO, WAJASIRIAMALI KUJIUNGA NA MFUKO HUO.

NSSF YAWAHIMIZA WACHIMBAJI WADOGO, WAJASIRIAMALI KUJIUNGA NA MFUKO HUO.

Na: Costantine James, Geita.

Wachimbaji wadogo wa madini pamoja na wafanya biashara mbalimbli mkoani Geita wametakiwa kujiunga na Mfuko wa hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa lengo la kujiwekea hakiba.

Hayo yamebainishwa na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma NSSF Lulu Mengele wakati akizungumza na wandishi wa habari Mkaoni Geita mara baada ya kutoa semina kwa wachimbaji wadogo pamoja na wajasiriamali mbalimbali.

Mengele amewataka wachimbaji wadogo pamoja na wajasiriamali mkoani Geita kuwa na desturi ya kujiwekea hakiba hasa katika Mfuko wa hifadhi ya Jamii (NSSF) ili ziweze kuwasaidia badae.

Meneja wa NSSF Mkoa wa Geita Winniel Lussingu amewataka wachimbaji wadogo pamoja na wajasiriamali hao kujiunga na mfuko huo ili waweze kukopesheka kupitia Banki ya Azania Banki pamoja na shirika la kuhudumia viwanhda vidogo (SIDO) kwa lengo la kukuza biashara zao .

Winniel amesema NSSF ni mfuko unaomjali kila mwananchi ikiwa ni pamoja na wajasiriamali wadogo katika kuhakikisha wanasaidiwa kujikuza kiuchumi kwa kupata mikopo ambayo ni nafuu kwani NSSF hutoa huduma bora wakati wote kwa mwanachama wake.

Meneja wa Azania Benki Mkoa wa Geita Rhoda Buluhya amesema Banki hiyo inafanya kazi kwa kushirikiana na NSSF Katika masuala ya utoaji wa mikopo kwa wachimbaji wadogo na wajasiriamali ili kuwawezesha kukuza mitaji yao.

Katibu tawala wa Mkoa wa Geita Prof. Godius kahyarara amewapongeza NSSF kwa huduma nzuri wanazitoa kwa wananchi amewataka kutoa elimu zaidi kwa wananchi ili waweze kujua faida za kujiunga na mfuko wa hifadhi ya Jamii (NSSF).

Previous articleKITUO CHA KUTIBU MAGONJWA YA MILIPUKO KUJENGWA KAGERA
Next articleTAMASHA LA JINSIA KANDA YA KASKAZINI LAFUNGWA SAME..DC MPOGOLO ATAKA SHERIA ZITUMIKE KUMALIZA UKATILI WA KIJINSIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here