Home LOCAL RAIS SAMIA ATAKA SHERIA KUTOA KIPAUMBELE KWA WANAWAKE

RAIS SAMIA ATAKA SHERIA KUTOA KIPAUMBELE KWA WANAWAKE

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapa Tuzo baadhi ya Waanzilishi wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika WiLDAF pamoja na vyeti kwa wadau waliofanikisha maendeleo ya Shirika hilo kwenye Maadhimisho ya miaka 25 ya kuanzishwa kwa Shirika hilo kwenye hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Oktoba, 2022. Wageni mbalimbali waliohudhuria Maadhimisho ya miaka 25 ya Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika WiLDAF kwenye hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Oktoba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali katika Maadhimisho ya miaka 25 ya Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) kwenye hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Oktoba, 2022. 

DAR ES SALAAM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania inahitaji Sheria madhubuti kuhakikisha kuwa wanawake wanashiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo na umiliki wa rasilimali.

Rais Samia amesema hayo leo kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (Women in Law and Development in Africa – WiLDAF) yaliyofanyika ukumbi wa Serena.

Aidha, Rais Samia amesema licha ya takwimu kuonyesha kuwa asilimia kubwa ya wanawake wanajishughulisha na shughuli za uzalishaji, bado baadhi ya mila na desturi zinawafanya wanawake kuendelea kukandamizwa.  

Rais Samia pia amesema Sheria ni nyenzo kuu ya ufikiwaji wa usawa wa kijinsia na ustawi wa wanawake hivyo kutoa kipaumbele kwa wanawake ni jambo la lazima ili kuleta maendeleo.

Vile vile, Rais Samia amesema ipo haja ya kufanya tathmini ya Sheria zilizopo na kuona zina mchango gani kwa Watanzania na kuhakikisha kuwa zinakwenda ngazi za chini ili ziweze kutambuliwa na kufahamika kwa wananchi.

Kwa upande mwingine, Rais Samia ametoa wito kwa Sheria kutungwa na kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ili kurahisisha kutoa elimu na ufahamu kwa wananchi.

Rais Samia ameiagiza Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum pamoja na Wasaidizi wa masuala ya Sheria kuwashirikisha wananchi na viongozi wa dini na kimila katika kuondoa vitendo vya udhalilishaji na ukandamizaji dhidi ya mwanamke.

Previous articleKIKAO CHA KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM CHAFANYIKA KISIWANDUI ZANZIBAR
Next articleRAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHUTUBIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA SHIRIKA LA WANANWAKE KATIKA SHERIA NA MAENDELEO BARANI AFRIKA (WildDAF) JIJINI DAR ES SALAAM
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here