Home BUSINESS MKURUGENZI WA STAMICO ATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI KWENYE MAONESHO YA...

MKURUGENZI WA STAMICO ATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance Mwasse leo  tarehe 02 Oktoba, 2022 ametembelea banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili mjini Geita .

Mara baada ya kupokea maelezo kutoka kwa wataalam wa Tume ya Madini amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Tume ya Madini hasa kwenye usimamizi wa Masoko ya Madini na Vituo vya Ununuzi wa Madini vilivyoanzishwa nchini.
 
“Endeleeni kuchapa kazi hasa kwenye utoaji wa elimu kuhusu fursa zilizopo kwenye Sekta ya Madini ili wananchi wengi waweze kushiriki huku Serikali ikipata mapato yake, hivyo Sekta ya Madini kuendelea kuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi,” amesisitiza Dkt. Mwasse.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here