Home LOCAL MAFUNZO KWA VITENDO KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO YAFANYIKA MOROGORO

MAFUNZO KWA VITENDO KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO YAFANYIKA MOROGORO

Na. WAF – Morogoro.

Matukio mbalimbali yakionesha mafunzo kwa vitendo namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo tishio la Ebola yakiendelea kwa wakufunzi ngazi ya Taifa kwa lengo la kwenda kutoa elimu katika Mikoa husika.

Mafunzo hayo yamemalizika leo Oktoba 16, 2022 katika Mkoa wa Morogoro, huku mambo muhimu katika mafunzo hayo ni pamoja na, jinsi ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Ebola, namna ya kuvaa na kuvua vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi kwa mtoa huduma pindi anapomhudumia mgonjwa wa Ebola pamoja na namna ya kutoa huduma kwa mgonjwa wa Ebola.

Mafunzo hayo yameanza kutolewa kwa Mikoa 12.

#MtuNiAfya
#JaliAfyaYako

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here