Home BUSINESS TASAC YATOA ELIMU KWA WANANCHI KATIKA MAONESHO YA TANO YA TEKNOLOJIA YA...

TASAC YATOA ELIMU KWA WANANCHI KATIKA MAONESHO YA TANO YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA

Afisa Masoko Mwandamizi wa Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)  Martha Kalvin (wa kwanza kulia) akikabidhi zawadi Kwa  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Bw. Msafiri  Mbibo  alipofanya ziara katika kutembelea Banda la Shirika hilo kwenye maonesho ya tano  Teknolojia ya madini yanayofanyika mkoani Geita.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Bw. Msafiri  Mbibo (kushoto) akisikiliza maelezo yanayotolewa na Afisa Masoko Mwandamizi wa Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)  Martha Kalvin (kulia) mara baada ya Mgeni huyo kufika katika Banda la Taasisi hiyo kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo.

Afisa Masoko Mwandamizi wa TASAC Martha Kalvin akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wengine wa Taasisi hiyo kwenye Banda lao.

Na: Hughes Dugilo, GEITA.

Afisa Masoko Mwandamizi wa  Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Kelvin amesema kuwa katika kutekeleza majukumu yao Shirika hilo limejikita katika kutoa elimu kwa wananchi kufahamu namna ambavyo shirika linavyotekeleza majukumu yake kwa mujubu wa sheria.

Ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum katika Maonesho ya tano ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayofanyika Mkoani Geita.

Amesema kuwa licha ya majukumu makubwa waliyonayo pia Shirika hilo limeendelea kutoa elimu kwa wananchi katika Maonesho hayo ili kufahamu namna  linavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria.

“TASAC tunashiriki maonesho ya tano mkoani Geita ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya majukumu yanayotekezwa Kisheria.  kama mdhibiti wa shughuli za usafiri kwa njia ya maji tunasimamia huduma zinazotolewa na Bandari, tunadhibiti na kusimamia ulinzi, usalama na utunzaji wa mazingira na kuratibu shughuli za uokoaji na utafutaji pale panapotokea dhoruba katika vyombo vya usafiri kwa njia ya maji”

“Pia tunatoa elimu kwa wananchi wa Geita hususani wadau wa Madini katika jukumu letu la kipekee kwenye biashara ya Meli ambapo kwa sasa tunafanya undoshaji wa shehena kwa makinikia na mashine zinazotumika katika migodi hivyo tunawakaribisha sana waweze kupata elimu zaidi itakayowasaidia kujua nini cha kufanya wanapotaka kuagiza mashine zao kuziingiza hapa nchini na kuzitoa pia na usafirishaji wa Makinikia” Ameeleza Martha.

Kwa mujibu wa Sheria, TASAC ina wajibu wa kusimamia kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhimiza usimmizi na shughuli za uwakala wa meli wenye ufanisi, kuhimiza shughuli za bandari na huduma za meli zenye ufanisi, kuhakikisha kunakuwepo usalama na ulinzi wa shehena, kuhimiza na kutunza mazingira, usalama na ulinzi wa bahari, maziwa na mito.

Aidha Shirika hilo pia lina wajibu wa kuhimiza ufanisi, uchumi na uaminifu, kuendeleza upanuzi wa sekta ya usafirishaji kwa njia ya maji, kuhimiza ushindani katika biashara ya uwakala wa meli, na kuingia kwenye majukumu ya kimkataba na watu wengine au kikundi cha watu.

Maonesho hayo ya Teknolojia ya Madini ni maonesho ya tano kufanyika Mkoani Geita yakiwa na lengo la kuwaleta pamoja wadau mbalimbali katika Sekta hiyo ili kubadilishana uzoefu wa kitaalamu na kujifunza Teknolojia za kisasa katika sekta hiyo pamoja na Taasisi nyingine ikiwemo TASAC.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here