Home SPORTS SIMBA YASONGA MBELE LIGI YA MABINGWA AFRIKA

SIMBA YASONGA MBELE LIGI YA MABINGWA AFRIKA

MABAO ya mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri dakika ya 29 na 50 yameipa Simba SC ushindi wa 2-0 dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Simba SC inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-0 kufuatia kushinda 2-0 pia kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Jijini Lilongwe nchini Malawi, Phiri akifunga moja na lingine, Nahodha, John Bocco.

Sasa vigogo hao wa Tanzania watakutana na mshindi wa jumla kati ya Primiero de Agosto ya Angola na Red Arrows ya Zambia katika Hatua inayofuata.

Mechi ya kwanza Agosto walishinda 1-0 nyumbani na leo watakuwa ugenini nchini Zambia.

Previous articleSUMAF WAKABIDHI MSAADA WA TAULO ZA KIKE 600 KWA WANAFUNZI BUGURUNI VIZIWI.
Next articleKAGERA, DODOMA JIJI ZATOSHANA NGUVU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here