Home SPORTS SIMBA SC, KMC HAKUNA MBABE

SIMBA SC, KMC HAKUNA MBABE

Na: Mwandishi wetu.

Klabu ya soka ya wekundu wa msimbazi Simba SC leo imetoshana nguvu na timu ya KMC kwa kutoka sare ya 2-2 katika mchezo wa ligi Kuu ya NBC.

Katika mchezo huo uliopigwa katika Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam timu ya Simba ilikuwa ya kwanza kuliona lango la KMC kwa goli la kuongoza likifungwa na mshambuliaji wake wa Kimataifa Moses Phil dakika za mwanzoni mwa mchezo huo.

Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko Simba ilikuwa ikiongoza kwa bao hilo huku timu zote zikionekana kuwa nguvu sawa.

Kipindi cha pili kilianza  kwa Kasi na mnamo dakika ya 47 kiungo mshambuliaji wa KMC Mateo Anthony alipachika bao la kusawazisha.

Katika dakika ya 58 ya mchezo huo George Makanga alipachika bao la pili ambapo Simba walisawazisha katika dakika za lala salama za mchezo huo goli likifungwa na mshambuliaji wake Abib kyombo.

Kufuatia matokeo hayo Kila timu imeondoka na alama 1 huku  Simba ikikusanya jumla ya alama 7  na magoli 7 zinazowafanya kukaa juu ya uongozi wa ligi.

Previous articleBALOZI SOKOINE AKUTANA NA MKUU WA IDARA YA UHAMIAJI WA SAUDI ARABIA
Next articleDC MBONEKO AKAGUA MIRADI YA MAJI VIJIJI VYA MWANDUTU, MWASHAGI INAYOTEKELEZWA NA RUWASA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here