Home LOCAL BALOZI SOKOINE AKUTANA NA MKUU WA IDARA YA UHAMIAJI WA SAUDI ARABIA

BALOZI SOKOINE AKUTANA NA MKUU WA IDARA YA UHAMIAJI WA SAUDI ARABIA

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amekutana kwa mazungumzo na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji wa Ufalme wa Saudi Arabia Luteni Generali Suliman Al-Yahya katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na Mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na namna ya kukuza ushirikiano baina pande mbili ambapo Saudi Arabia imeonyesha utayari wa kujadiliana na Serikali ya Tanzania juu ya upatikanaji viza za kuingia nchini Saudi Arabia.

Kwa upande wake, Balozi Sokoine ameishukuru Serikali ya Saudi Arabia kwa kutoa ushirikiano kwa Tanzania katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kijamii na kiuchumi.

Balozi Sokoine ametumia mazungumzo hayo kuelezea utayari wa Tanzania kuingia makubaliano ya kuanzishwa Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika kusimamia utekelezaji wa masuala mbalimbali ya ushirikiano.

Previous articleMEYA KUMBILAMOTO AMEAGIZA WATUMISHI WALIOSIMAMISHWA MACHINJIO VINGUNGUTI WACHUNGUZWE
Next articleSIMBA SC, KMC HAKUNA MBABE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here