Home LOCAL MTENDAJI MKUU WA GLOBAL FUND AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

MTENDAJI MKUU WA GLOBAL FUND AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

Mtendaji Mkuu wa Global Fund, Mfuko wa kupambana na Virusi vya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria Bw. Peter Sands amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ikiwa ni pamoja na kuona utekelezaji wa afua za mapambano dhidi ya magonjwa hayo.

Bw. Peter Sands amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. John Jingu pamoja na Dkt. Catherine Joachim Mkuu wa Sehemu ya Maboresho katika na Sekta ya Afya kutoka Wizara ya Afya ambaye anasimamia uboreshaji wa huduma kupitia Miradi ya Global Fund.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here