Home LOCAL WADAU WA HABARI WANATAMANI KUONA SHERIA YA HABARI INAKUWA RAFIKI: MEENA

WADAU WA HABARI WANATAMANI KUONA SHERIA YA HABARI INAKUWA RAFIKI: MEENA

NEVILE Meena, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) amesema, sehemu ya Sheria ya Habari ya Mwaka 1976, kwa miaka 40 ilitoa mwanya kwa mtu mmoja kuamua kufungia chombo cha Habari kwa matakwa yake.

Na kwamba, hata kwenye mabadiliko ya sheria yaliyofanywa mwaka 2016, uhalali wa utashi wa mtu mmoja kufungia chombo cha habari ulirejeshwa bila kujali athari zake.

Ni kauli ya Neville Meena, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), akizungumza katika Kipindi cha Front Page kinachorushwa na Radio pia Global Televisheni leo tarehe 13 Septemba 2022, jijini Dar es Salaam.

‘‘Sheria ya Habari ya Mwaka 1976, imefanya kazi kwa miaka 40, muda wote huo imetoa mwanya kwa mtu mmoja (waziri) kufungia chombo cha habari anapojisikia kufanya hivyo.

‘‘Hata Sheria ya Habari ya Mwaka 2016 ilipotungwa, imefuata mkondo huo huo wa kutoa mamlaka kwa mtu mmoja kuamua kufungia chombo cha habari ama la ingawa mamlaka hayo amepewa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Malelezo! Katika mabadiliko haya, tumeiomba serikali iondoe kipengele hicho,’’ alisema Meena.

Alisema, Sheria ya Mwaka 2016 ilianza kulalamikiwa kwa kuwa, haikuondoa mitego iuliyowekwa na sheria mwa mwaka 1979, na zaidi imechangia kudumaa kwa vyombo vya habari nchini.

Alisema, baada ya wadau wa Habari kupiga kelele, Serikali ya Awamu ya Sita iliona haja ya kukjaa meza mod ana wadau wa habari ili kupatia ufumbuzi.

Na kwamba, hatua za awali alizochukua Rais Samia Suluhu Hassan, ziliongeza ari ya wadau wa habari kushirikiana ili kung’oa vipengele hasi vya sheria ya habari.

‘‘Mwaka jana mwishoni mwa mwezi wa sita, tulikutana na rais (Rais Samia) na akasema, yupo tayari kushughulikia malalamiko yetu.

‘‘Hatua zilianza kuchukuliwa kwa serikali kuleta mapendekezo ya maeneo ya kurekebisha, lakini na sisi tuliongeza yetu ambayo wao walikuwa hawajaweka kwenye mapendekezo yao.

Pia alisema, wadau wa Habari wanachopambana ni kuhakikisha inapatikana sheria rafiki kwa wanahabari na wamailiki wa vyombo vya habari nchini.

Alisema, ingawa kuna baadhi ya sheria zinaozonekana kuwa mbaya hazijatumika, sheria hizo hazipaswi kuwepo kwa kuwa zinatoa mwanya kwa anayetaka kuzitumia kufanya hivyo.

‘‘Kuna sheria zingine zipo na inaelezwa hazijatumika, sheria kama hizo hazipaswi kuwepo maana kuwepo kwake, anaweza kutokea mtu mmpja akazitumia na tukawa hatuna cha kusema.

‘‘Kikubwa katika tasnia ya habari ni kila mmoja atekeleze majukumu yake, serikali ibaki na majukumu yake na wanahabri kama wanataaluma wabaki na majukumu yao,’’ alisema.

Meena alitoa mfano kwamba, kuna baadhi ya magazeti yalilalamika kuandika vibaya lakini hayakuwahi kufungiwa, lakini mengine yalifdungiwa kwa kuwa tu, sheria ya kufanya hivyo ilikuwepo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here