Home LOCAL ALIYOSEMA NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII AMBAYE PIA NI MBUNGE WA...

ALIYOSEMA NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII AMBAYE PIA NI MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MWANZA, MHE. MARY MASANJA KATIKA HAFLA YA UFUNGUZI WA STENDI YA KISASA YA MABASI YA NYAMHONGOLO MANISPAA YA ILEMELA JIJINI MWANZA LEO SEPTEMBA 13,2022

• Wakazi wa Mwanza tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo ametoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo na ya kimkakati ambayo inaenda kuinua uchumi wa wakazi wa hapa na watanzania wote kwa ujumla.

• Miradi ya Kimkakati inaenda kuifungua Mwanza kiutalii na ikizingatiwa hivi karibuni Mhe. Rais amezindua filamu ya Royal Tour hivyo tunatarajia kupokea wageni wengi hapa nchini kwa mfano Uwanja wa Ndege, Stendi ya Mabasi ya Nyamhongolo itasaidia kuvutia watalii kutembelea vivutio vyetu.

• Mhe. Makamu wa Rais tunatambua kwamba umekuwa ukituelekeza kuhifadhi na kutunza mazingira , hivyo sisi wakazi wa Mwanza tumeanza upandaji wa miti ili kuwepo hali ya hewa nzuri na mazingira bora ili wageni wanapokuja katika mkoa wetu waone mandhari nzuri.

• Tupelekee salamu zetu kwa Mhe. Rais na tunamuahidi kwamba tutaendelea kushirikiana bega kwa bega kuipeleka Tanzania mbele.

Previous articleWADAU WA HABARI WANATAMANI KUONA SHERIA YA HABARI INAKUWA RAFIKI: MEENA
Next articleMAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 14-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here