Home SPORTS KIDUKU AMTWANGA KHALED MTWARA

KIDUKU AMTWANGA KHALED MTWARA

Bondia Twaha Kiduku amefanikiwa kushinda pambano  lake la Kimataifa dhidi ya Bondia wa Kimataifa raia wa Misri Abdo Khaled na kuondoka na mikanda miwili kwa pamoja.

Katika Pambano hilo lililopigwa katika uwanjwa wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara lilikuwa na ‘Raund’10 lililojumuisha mapambano mengine ya utangulizi.

Baada ya mchezo huo Kiduku aliwashikuru watanzania kwa kumuunga mkono na kusema kuwa ushindi wake ni ushindi wa watanzania wote na heshima kwa Taifa la Tanzania.

“Ushindi huu ni wa Tanzania na wananchi wote kwa ujumla, nilimuahidi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kuwa lazima niache heshima Mtwara Ili iwakilishe nchi nzima” amesema Kiduku.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here