Home SPORTS KIDUKU AIBUKA MBABE DHIDI YA KHALED

KIDUKU AIBUKA MBABE DHIDI YA KHALED

Mwandishi Wetu, Mtwara

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Twaha Kiduku amefanikiwa kushinda mkanda na kuwa bingwa mpya wa UBO Intercontinental pamoja na kutetea mkanda wake wa ubingwa wa UBO Afrika uzani wa Super Middle dhidi ya Abdo Khaled wa Misri.

Katika pambano hilo ambalo limepigwa juzi usiku kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona uliopo mjini hapa ambapo pambano hilo limechezwa kwa raundi kumi.

Kiduku ambaye alikutana mpinzani mkali na mwepesi katika kukimbia kwenye sehemu zenye madhara upande wake kutokana na ubora wa aliokuwa akionyesha Kiduku katika pambano hilo kabla ya kushinda kwa pointi.

Kiduku amewashukuru kufanikiwa kushinda ubingwa huo kutokana na sapoti kubwa aliopewa na serikali ya mkoa wa Mtwara kabla na baada ya pambano hilo huku akitoa zawadi ya ushindi huo kwa mtoto wa mfanyabiashara Said Salim Bakharesa.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa Mtwara, Kanali Ahmed Abasi amepongeza bondia huyo kutokana na ushindi huo pamoja na pambano hilo kufanyika mkoani hapa huku akimtaka kuendeleza kuutangaza mkoa huo.

Mbali ya pambano la Kiduku, bondia Karim Mandonga pambano lake haliweza kupatikana mshindi kutokana na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini ‘TPBRC’ chini ya rais wake, Chaulembo Palasa kulifuta kufuatia kuwepo makosa ya kisheria kutoka kwa mwamuzi wa pambano hilo, Habib Mkarafuu kufanya makosa ya kimsingi.

Wengine, Adam Lazaro amefanikiwa kumchapa kwa pointi Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ katika pambano la raundi kumi wakati Ibrahim Tamba akifanikiwa kumpiga Alto Kyenga, Joseph Mchapeni ameendeleza utemi wake kwa Pascal Manyota kufanikiwa kumpiga kwa pointi wakati Bosco Bakari wakitoka sare na Malik Deo wa Mwanza sawa na Mrisho Mzelele dhidi ya Karim Omari.

Fundi, Emilian Polino amefanikiwa kumchapa Osama Arabi wa Mtwara wakati Nasra Msami akimpiga Halima Bandora huku Shaban Ndaro akimpoteza kwa kipigo kizito mkongwe Seleman Galile.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here