Home SPORTS KANAL HEMED AZINDUA TIKETI ZA KIDUKU MTWARA

KANAL HEMED AZINDUA TIKETI ZA KIDUKU MTWARA

Na: Mwandishi wetu, Mtwara.

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abass juzi ameufungua mkoa wa Mtwara kwa kuzindua uuzaji wa tiketi za kuelekea katika pambano la Mtwara Ubabe Ubabe 2 linalotarajia kupigwa Septemba 24, mwaka huu mkoani hapa huku akimtakia ushindi mkubwa bondia Mtanzania, Twaha Kiduku atazichapa dhidi ya Abdo Khaled wa Misri.

Kiduku atapanda ulingoni kutetea mkanda wake wa ubingwa wa UBO katika uzani wa Super Middle kwenye pambano hilo litakalopigwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoa hapa.

Katika uzinduzi huo mkuu wa mkoa huo alinunua tiketi za Sh laki mbili kwa lengo la kuhamasisha wananachi na wadau wengine kujitokeza kununua tiketi za pambano hilo linalosubiriwa na wakazi wa mkoani hapa.

Mara baada ya Kanali Ahmad alisema kuwa ameshiriki katika kuufungua mkoa wa Mtwara na uzinduzi wa tiketi za pambano la Mtwara Ubabe Ubabe 24 litakalofanyika Septamba 24, mwaka huu kwa kuwataka wananchi wajitokeze kushiriki pamoja na ununuaji wa tiketi za pambano hilo.

“Jioni ya leo (juzi) nimeshiriki katika zoezi la kuufungua mkoa wa Mtwara sambamba na uzinduzi wa ununuaji wa tiketi kwa ajili ya pambano la Septamba 24 ambalo litafanyika kwenye mkoa wetu wa Mtwara, wito wangu kwa wananchi tushiriki na tujitokeze kwenye ununuzi wa tiketi za pambano ila baada ya hapo tutakuwa na muendelezo wa siku ya utalii duniani, tufanya utalii wa ndani ya mkoa Septemba 27.

“Niendelee kusisitiza wananchi kujitokeza kwenye shughuli hiyo na kuwashughukuru wadau wa maendeleo kujitokeza kusapoti juhudi hizi za maendeleo, wito wangu watu wote wanaoweza kuja kushiriki waje lakini pia nitakie kila la kheri Kiduku katika pambano hilo kwa kuwa ni Mtanzania mwenzetu aweze kushinda,” alisema Kanali Ahmed.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here