Home BUSINESS DC ILALA APIGA MARUFUKU UUZAJI NYAMA KIHOLELA KAMA NYANYA VINGUNGUTI

DC ILALA APIGA MARUFUKU UUZAJI NYAMA KIHOLELA KAMA NYANYA VINGUNGUTI

Na: Heri Shaaban (Ilala)

MKUU wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija AMEPIGA MARUFUKU Wafanyabiashara wa Machinjio ya kisasa Vingunguti kuuza nyama kama mafungu ya nyanya Barabarani badala yake amewataka Wafanyabiashara wote kuuza nyama hizo kwa kufuata utaratibu wa Serikali katika MABUCHA ya kisasa yaliojengwa kwa fedha za Serikali.

Mkuu wa Wilaya Ludigija alitoa tamko hilo katika ziara yake katika MABUCHA hayo ya kisasa baada kuwamisha Wafanyabishara kuwaelekeza hapo kuanza rasmi kufanya Biashara katika Mazingira salama .

“Napiga marufuku kuuza nyama Barabarani kama nyanya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Rais Samia Suluhu Hassan, imewajengea mabucha haya Sasa yamekamilika mnatakiwa kufurahia matunda ya Serikali yenu sio kufanya Biashara katika Mazingira sio Salama hii haikubariki “alisema Ludigija .

Ludigija aliagiza Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo na Afisa Mtendaji kusimamia Wafanyabishara wasifanye Biashara katika Barabara ya Vingunguti badala yake wote wawe katika sehemu rasmi ambazo Serikali imejenga mabucha .

Mkuu wa Wilaya Ludigija alisema Sasa hivi Vingunguti kitovu cha Biashara mabucha hayo yatapanuliwa eneo kubwa zaidi na Serikali ina mpango wa kulipa fidia baadhi ya nyumba zilizo mbele ya mabucha hayo Ili yawe wazi na kujenga eneo la kupaki magari na kituo Cha daladala .

Aliwapongeza Wachinjaji wa Vingunguti kutii agizo la Serikali wote kukubali kuuza nyama katika mabucha ya kisasa ambapo aliongozana na wakuu wa Idara wote kila mmoja kuangalia KERO yake Ili kutatua kwa haraka .

Aidha pia alimwagiza Mhandisi wa Halmashauri kukaa na Mkandarasi kuanza kuanza ujenzi wa jengo lingine kwa ajili ya mabucha

Pia alikagiza watenge chumba kimoja kwa ajili ya kuchukua Hoda za wateja wa mahoteli makubwa baadae kuwasambazia wateja.

Aliwataka wazingatie usafi Ili machinjio yapendeze kwa ajili ya kujilinda na kipindupindu ambacho kimeingia katika baadhi ya mikoa .

Ludigija alisema mabucha ya Vingunguti tayari yamefunguliwa rasmi na Wafanyabiashara wanafanya Shughuli zao amesema kukiwa na changamoto Ofisi yake ya Wilaya ipo wazi kila Alhamis ametenga siku Maalum ya kusikiliza kero za Wananchi wa Wilaya ya Ilala .

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here