Home LOCAL RC GEITA, APIGA MARUFUKU WATOTO KUFANYA KAZI MIGODINI.

RC GEITA, APIGA MARUFUKU WATOTO KUFANYA KAZI MIGODINI.

Wakwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela kati kati ni Afisa Elimu Mkoa wa Geita Mwl. Antony Mtweve na wa Mwisho ni Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Martha Mkupasi.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela.

Na. Costantine James, Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela amepiga marufu watoto wadogo kujihusisha na shaghuli za migodini katika mkoa wa Geita na badala yake wajikite katika masomo.

Mhe. Shigela amesema hayo katika uzinduzi vitabu vya mwongozo wa Kuboresha Usimamizi wa Elimu kwa mkoa wa Geita ambavyo ni pamoja na kitabu cha Mwongozo wa Mkakati wa kuimarishaji Ufundishaji na Ujifunzaji Ngazi ya Elimu Msingi, Kitabu cha Changamoto katika Uboreshaji wa Elimu msingi na Sekondari nini kifanyike? pamoja na Kitabu cha Mwongozo wa Uteuzi wa Viongozi wa Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mikoa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela amesema katika mkoa wa Geita kuna changamoto ya watoto wadogo kujihusisha na shughuli za migodini hali inayochangia kuongezeka kwa utoro shuleni na kupelekea watoto hao kukosa haki yao msingi ya kupata elimu.

Amewaagiza Wakuu wa wilaya, watendaji wa kata pamoja na vijiji kuhakikisha wanasimamia vyema watoto wasionekane katika maeneo ya Migodi ili kuhakikisha watoto hao wanakuwa shuleni kwa ajiri ya kupata elimu. ndani ya maeneo yao.

Amewataka walimu, maafisa elimu kata shule za msingi pamoja na sekondari kusimamia vyema mwongozo huo wa elimu uliotolewa ili kuboresha hali ya elimu ndani ya mkoa kwa lengo la kuongea ufaulu kwa mwanafunzi.

Mhe, Shigela amezitaka halmashauri ndani ya mkoa huo kutenga bajeti kwa ajiri ya kuwapa motisha wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo yao kwa lengo la kuchochea na kuhamasisha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao.

Kwa upande wake afisa elimu Mkoa wa Geita Mwl. Antony Mtweve amesema changamoto ya utoro wa wanafunzi katika mkoa wa Geita bado ni kubwa hivyo kupitia miongozo hiyo iliyozinduliwa na Mkuu wa mkoa, wao kama mkoa wanaenda kuitekeleza vyema pamoja na kuunda mikakati mbalimbali kwa lengo la kutokomeza utoro kwa wanafunzi katika mkoa wa Geita.

Previous articleMAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 9-2022
Next articleDC ILALA APIGA MARUFUKU UUZAJI NYAMA KIHOLELA KAMA NYANYA VINGUNGUTI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here