Home LOCAL ACT WAZALENDO YATOA MAAZIMIO YA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU

ACT WAZALENDO YATOA MAAZIMIO YA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU

Halmashauri Kuu ya chama cha ACT wazalendo imepitisha Azimio la kuundwa kwa Kitengo cha Chama cha Kusimamia Uwajibikaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambapo Kitengo hicho kitakuwa na majukumu ya kufuatilia kwa karibu uwajibikaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kutoa sera mbadala.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu maadhimio ya kikao cha halmashauri kuu ya ACT wazalendo iliyoketi jana Septemba 4, Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma Janeth Joel Amesema Halmashauri Kuu ilipokea Taarifa ya Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Chama kwa
upande wa Bara na Zanzibar.

Halmashauri Kuu imepongeza hatua hiyo iliyofikiwa kwa sasa ya kupatikana kwa Ofisi ya Wasemaji wa Kisekta (iliyopo Oysterbay, Dar es salaam) na Ofisi ya Makao Makuu (iliyopo Magomeni, Dar es salaam) iliyopewa jina la Jengo la Marehemu Maalim Seif ikiwa ni kumuenzi aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho. Nakuongeza kwamba Halmashauri Kuu imeielekeza Sekretarieti kufanya uzinduzi wa Ofisi hiyo Mpya ya Makao makuu kufanyika mapema iwezekanavyo.

Halmashauri Kuu ya Chama Taifa pia imepitisha Sera ya Chama cha Wamachinga inayoangazia kutatua madhila na changamoto zinazowakabili wamachinga na hatua za kisera zinazopaswa kuchukuliwa kukabiliana na changamoto hizo.

Aidha Halmashauri kuu imepitisha ratiba ya Uchaguzi wa Ndani ya Chama kwa Ngazi za Matawi, kata, Majimbo, Mikoa na Taifa kuanzia kufanyika machi 2023 hadi 2024.

Chama pia kimepokea Taarifa ya Mageuzi ya Uendeshaji wa Chama Kisasa kupitia mfumo wa ACT Kiganjani na kutoa maelekezo mahususi ya kuendelea kujiimarisha katika utumiaji wa njia za kidijitali katika uendeshaji wa Chama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here