Home BUSINESS UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA BRELA KWA NJIA YA MTANDAO UMERAHISISHA WANANCHI KURASIMISHA...

UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA BRELA KWA NJIA YA MTANDAO UMERAHISISHA WANANCHI KURASIMISHA BIASHARA ZAO

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kutoka BRELA, Bi. Rhoida Andusamile alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Tano ya Teknolojia ya Madini Madini yanayofanyika Mkoani Geita.

Na: Hughes Dugilo, GEITA.

Wakala wa usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeeleza kuwa upatikanaji wa huduma kwa njia ya mtandao umewarahisishia wananchi kurasimisha biashara zao na kupata taarifa muhimu popote pale walipo.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kutoka BRELA, Bi. Rhoida Andusamile alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Tano ya Teknolojia ya Madini Madini yanayofanyika Mkoani Geita.

Amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa huduma ya usajili kwa njia ya mtandao ( Online Registration System-ORS) kumekuwa na mwamko kwa watanzania kurasimisha biashara zao.

“Huduma za usaji kwa njia ya mtandao imewezesha kwa kiasi kikubwa wananchi kupata huduma za BRELA popote walipo,” amefafanua Bi Andusamile.

Aidha ameongeza kuwa mbali na kutumia vyombo vya habari mbalimbali wameendelea kutumia mitandao ya kijamii kuelimisha wananchi juu ya huduma mbalimbali za BRELA ili kuwa na uelewa wa pamoja.

“Hatuko nyuma kwenye suala la mitandao ya kijamii, tunaitumia ipasavyo kuhakikisha wananchi wanaelewa huduma tunazotoa,” ameongeza Bi. Andusamile.

Aidha amewasihi watanzania kurasimisha biashara zao kwa njia ya mtandao kwa kuingia kwenye wovuti ya BRELA.

“Mfanyabiashara anaposajili Jina la Biashara ama Kampuni, huaminika mahali popote na kupata fursa mbalimbali za kibiashara,” ameeleza.

MWISHO

Previous articleWADAU SEKTA YA NGUO AINISHENI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI ILI ZIFANYIWE KAZI: DKT KIJAJI
Next articleWACHIMBAJI WADOGO MSITUMIE WAGANGA WA JADI KWENYE UCHIMBAJI WA MADINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here