Home BUSINESS WADAU SEKTA YA NGUO AINISHENI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI ILI ZIFANYIWE KAZI: DKT KIJAJI

WADAU SEKTA YA NGUO AINISHENI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI ILI ZIFANYIWE KAZI: DKT KIJAJI

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe  Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.)  amewashauri wadau wa sekta ya nguo kuainisha changamoto za kisera, kikodi na kiutendaji wanazokutana nazo ili azifanyie kazi.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Sepetemba 26, 2022 jijini  Dodoma alipokutana na wadau wa sekta ya nguo na  walio chini ya Chama cha Wazalishaji Nguo na Mavazi Tanzania (TEGAMAT) ili kujadili changamoto wanazokutana nazo.

Aidha, Waziri Kijaji amewashauri wadau hao kutokufunga viwanda, kwa kuwa ni sekta inayotoa ajira nyingi kwa vijana.

“Njoni tukae tuongee, tupange kwa.pamoja tuone cha kufanya, tunataka viwanda vifanye kazi katika Serikali ya Awamu ya Sita amnayo ni sikivu”.  Amesema Dkt. Kijaji.

Aidha ameongeza  kuwa nia ya Serikali ni kuona viwanda nguo vya Tanzania vinakua shindani  na vinahudumia  Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Akiongea mbele ya Waziri Kijaji, Katibu Mtendaji  wa TEGAMAT Bw. Adam Zuku ameomba kuwe na ushindani wa haki na usawa kati ya waingizaji vitenge na wazalishaji ili waweze kushindana katika soko la nje.

“Tunatamani kuhudumia soko la SADC,EAC, ACFTA” alisema Zuku.

Aidha, Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau hao wameiomba Serikali kuanzisha mitaala ya nguo kwa kuwa kwa sasa kuna uhaba wa wataalamu hao.

Pia  wameiomba tozo zinazotozwa na Taasisi mbalimbali za Serikali kujumuishwa kwa pamoja ili kuwapunguzia usumbufu na gharama kubwa za uendeshaji.

Previous articleMAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 30-2022
Next articleUPATIKANAJI WA HUDUMA ZA BRELA KWA NJIA YA MTANDAO UMERAHISISHA WANANCHI KURASIMISHA BIASHARA ZAO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here