Home SPORTS ‘NUNGUNUNGU MASTER’ AINUA SHANGWE MSIMBAZI AKIFUNGA BAO PEKEE LA USHINDI

‘NUNGUNUNGU MASTER’ AINUA SHANGWE MSIMBAZI AKIFUNGA BAO PEKEE LA USHINDI

KLABU ya wekundu wa Msimbazi Simba SC imeitandika timu ya Tanzania Prison bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu uliochezwa leo katika Dimba la Sokoine Jijini Mbeya.

Bao pekee la kiungo mkabaji wa Simba Nungunungu master Jonas Mkude lililopatikana dakika ya 86 liliifanya timu ya Simba kutoka kifua mbele kwa kukusanya alama 3 muhimu ambapo hadi filimbi ya mwisho ya mchezo huo simba iliibuka kwa bao hilo pekee.

kufuatia mchezo huo timu ya simba imeweka kibindoni alama 10 katika msimamo wa ligi kuu ya NBC na kukwea mpaka nafasi ya pili ikiwa nyumba ya washindani wao wa karibu timu ya Yanga inayoonga ligi hiyo kwa magoli mengi ya kufunga.

Previous articleMAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI BUTIMBA MWANZA
Next articleMAKAMU WA RAIS AKIHITIMISHA ZIARA JIJINI MWANZA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here