Home BUSINESS BRELA YAWAITA WADAU KUTOA MAONI MAREKEBISHO YA SHERIA YA LESENI ZA BIASHARA,...

BRELA YAWAITA WADAU KUTOA MAONI MAREKEBISHO YA SHERIA YA LESENI ZA BIASHARA, SURA 208

Mkurugenzi  wa  leseni   kutoka Wakala  wa Usajili  wa   Biashara  na  Leseni  ( BRELA)  Andrew  Mkapa akizungumza wakati alipokuwa akifungua kikao kati ya  Wakala  wa Usajili  wa   Biashara  na  Leseni  ( BRELA) pamoja  na  Taasisi  za  Sekta  za  Umma  ili  kupata  maoni  na mapendekezo  ya   Mabadiliko   ya   Sheria  ya  leseni  za  Biashara  ya  mwaka  1972.

Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Leseni za Biashara wa BRELA Tawi Kilemile akiwasilisha mada ya Mpendekezo ya marekebisho ya Sheria ya Leseni za Biasara, sura 208 katika kikao cha kukusanya maoni ya wadau kuhusu marekebisho ya Sheria ya leseni za Biashara, sura 208 Kilichofanyka leo Jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi  wa  leseni   kutoka Wakala  wa Usajili  wa   Biashara  na  Leseni  (BRELA)  Andrew  Mkapa (katikati aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na kikosi kazi cha kuratibu ukusanyaji maoni ya wadau kuhusu marekebisho ya Sheia hiyo.

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Wakala wa usajili wa Leseni na Majina ya Biashara (BRELA) umezindua rasmi zoezi la kupokea maoni ya wadau juu ya mapendekezo ya marekebisho ya Sheria  ya  leseni  za  Biashara  ya  mwaka  1972.

Uzinduzi huo umefanyika leo Septemba 14,2022 Jijini Dar es Salaam ambapo wadau mbalimbali walikutana na kuipitia Sheria hiyo ili kufahamu maeneo gani katika sheria hiyo na kutoa mapendekezo yako ya marekebisho katika Sheria hiyo.

Akizungumza wakati wa kufungua  rasmi zoezi hilo Mkurugenzi  wa  leseni   kutoka Wakala  wa Usajili  wa   Biashara  na  Leseni  (BRELA)  Andrew  Mkapa  amesema  kuwa kupitia   kikao   hicho  kutawezesha  kupata  mchango   utakaofanikisha    maboresho   ya    Sheria hiyo ili kuifanya iendane na mazingira ya sasa ya kufanya biashara pamoja na kanuni mbalimbali zinazopaswa kufanyiwa marekebisho.

“kupitia   kikao   hiki  kutawezesha  kupatikana kwa michango   itakayofanikisha  maboresho  ama   marekebisho    ya    Sheria  ya  leseni  za  Biashara Sura  208   ambayo   imeonekana  kupitwa   na  wakati” 

“Sheria iliyopo  kwa  sasa  haiendani   na  mazingira   ya  wakati  huu na  imeonekana   kuwepo   na  mikwamo  kadhaa  kutokana   na  Mabadiliko  ya  Teknolojia  ya  Ufanyaji  Biashara  ikiwemo Biashara za mtandaoni ambazo Sheria hii haiwagusi kabisa”amesema Mkapa.

Ameongeza kuwa mkutano huo utadumu kwa siku tatu na kupokea maoni kutoka kwa wadau wa Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi kisha kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu kijaji juu ya mchakato huo watakaa na kuyachakata maoni hayo ili kupata sheria inayokidhi matakwa ya wote.

Kwa   upande  wake  Afisa  Biashara   kutoka  Wizara  ya  Uwekezaji, Viwanda  na  Biashara (WUVB) Denis  Mzamiru  amesema   kinachowasukuma   kufanya  maboresho  na   Marekebisho  ya  Sheria   hiyo   ni   pamoja  na   kuifanya   Sheria  kuendana  na  Mazingira  ya   sasa   ya  ufanyaji   Biashara  ikienda  sambamba   na  uwepo   wa  urahisi  na  wepesi   kwa  wafanyabiashara  kupata  leseni  za  Biashara.

Previous articleMAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 14-2022
Next articleMAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI BUTIMBA MWANZA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here