Home LOCAL TARURA ILALA YATENGA BAJETI SHILINGI BIL 25.2 ZA BARABARA

TARURA ILALA YATENGA BAJETI SHILINGI BIL 25.2 ZA BARABARA

Na: Heri Shaaban (Ilala)

WAKALA wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) wilaya ya Ilala imetenga bajeti ya shilingi Bilioni 25.2 kwa ajili ya Barabara kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Wilayani Ilala .

Hayo yalisemwa na Meneja wa TARURA wilaya ya Ilala Silvester Chinengo, katika Baraza la Madiwani Halmashauri ya Jiji Dar es Salaam wakati wa kuwasilisha Taarifa katika baraza la Jiji hilo.

Meneja Silvester alisema katika Bajeti hiyo ya 2023 kila Jimbo fedha za Mfuko wa Jimbo wametenga shilingi milioni 500 Jimbo la Segerea na Ukonga na Jimbo la Ilala wametengewa shilingi milioni 640 za Barabara za Barabara fedha za Mfuko wa Jimbo

Aidha Meneja alisema pia Serikali imetoa shilingi milioni 500 ,000,000.00 Jimbo la Segerea na Ukonga kwa ajili ya BARABARA na Jimbo la Ilala wametenga shilingi 2,800,000,000.00 kwa ajili ya BARABARA fedha hizo zimetokana na tozo ya Mafuta .

Akizungumzia Utekelezaji wa kazi za Ujenzi na matengenezo ya BARABARA na madaraja kwa mwaka 2022/ 2023 wakala amekamilisha mchakato wa Manunuzi kwa miradi asilimia 60 ya Bajeti ya miradi asilimia 40 ya Bajeti ipo katika mchakato wa Manunuzi ambayo ni awamu ya pili ya Manunuzi .

“Miradi ya fedha za mapato ya ndani kutoka kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inasubiri kupitishwa kwa mpango kazi wa Utekelezaji “ alisema Silvester .

Akizungumzia Changamoto alisema katika kushughulikia ujenzi wa matengenezo ya Mtandao wa Barabara wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ifinyu wa bajeti .

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here