Khalid Msabaha Mratibu wa Sensa Mkoa wa Geita.John I.John Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale Geita
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale Geita
Na. Costantine James, Geita.
Mratibu wa zoezi la Sensa ya watu na makazi Mkoa wa Geita Bw. Khalid Msabaha amesema zoezi hilo kwa sasa linaendelea vizuri na hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza katika mkoa huo hivyo wanaendelea vizuri kuwahesabu wakazi wa Geita.
Akizungumza na Greenwaveblog Bw. Khalid amesema mpaka sasa zoezi la Sensa ya watu na makazi Mkoa wa Geita limefikia asilimia 50% na wanaendelea na zoezi hilo ili kuhakikisha kila mtu anahesabiwa.
‘’Bado tunaendelea kuwahesabu watu kwenye maeneo mbalimbali na hatujakutana na mkwamo wowote wakutukwamisha tunakwenda vizuri kwa asilimia tumeshafika asilimia 50%” amesema Khalid Msabaha Mratibu wa Sensa mkoa wa Geita.
Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale ndugu John I. John amewataka madiwani wa halmashauri hiyo kuendelea kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya watu na makazi linaloendelea hapa nchini.
Ametoa rai hiyo wakati wa kikao cha baraza la madiwani wa wilaya ya Nyang’hwale wakati wa kujadili taarifa mbalimbali za kata amesema madiwani wahakikishe wanashiriki vyema katika zoezi la senza ili kuwezesha kufakikisha zoezi hilo kama ilivyokusudiwa.
Amesema madaiwani wanayonafasi kubwa katika jamii hivyo hawana budi kutimia nafasi zao katika kuendeleza kutoa hamasa kwa wananchi ili waweze kujitokea kwa wingi kuhesabiwa pamoja na kutoa ushirikiano.
John amesema viongozi wanapaswa kuonyesha juhudi kubwa katika zoezi hilo ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassani aliyewezesha kufanikisha kwa zoezi la sense ya watu na makazi hapa nchini. wa kutosha kwa makarani wa Sensa.
“Mimi nimehesabiwa wewe je? Kwa wale ambao bado hawajahesabiwa tuhakikishe zoezi hili linafanyika vizuri kwahiyo sisi viongozi lazima tuunge juhudi za mhe Rais Samia Suluhu Hassani ili kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa vizuri’’ Amesema Bw. John John.
Nao baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale wamesema tangu kuanza kwa zoezi hilo wao kama viongozi kazi ya kata wanashiriki kikamilifu katika kuwahamasisha wananchi kushiriki katika zoezi hilo ili kuwezesha kufanyika kwa ufanisi pamoja na kufikia malengo kama Mhe, Rais Samia alivyokusudia.
Zoezi la sense ya watu na makazi linaendelea na leo ni siku ya nne mfululizo tangu zoezi hilo lilipoanza Augusti 23, 2022 na linatarajiwa kukamilika Augusti 30,2022.