Timu ya Mpira wa Kikapu kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania iliyokuwa inashiriki Mashindano ya Majeshi ya Dunia imeshika nafasi ya Nne Kati ya Nchi 23 zilizoshiriki Mashindano hayo nchini Ujerumani.
Katika Mchezo wa Nusu Fainali Tanzania ilipoteza na Ufaransa kwa Vikapu 21 kwa 10 kabla ya kufungwa na Marekani
Katika kusaka Mshindi wa Tatu kwa Vikapu 21 kwa 13.
Nafasi ya Kwanza imechukuliwa na Lithuania ikifuatiwa na Ufaransa na nafasi ya Tatu imenyakuliwa na Ufaranssa.
Aidha, Kamati ya ufundi inayoongozwa na Rais wake Luteni Kanali Tom Bellairs imechagua timu ya Tanzania kuwa ni timu bora na kupewa kikombe cha Nidhamu ( CISM Fair play Trophy).
Pia Koplo Baraka Sadick amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano ( MVP) huku Meneja Kapteni Mohamed Kasui na Kocha Sajenti Taji Haleluya Kavalambi wamechaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati ya ufundi.
Timu ya Kikapu ya JWTZ ilishiriki Mashindano Kama hayo Mwaka 1993 na kutolewa katika Hatua za Awali.
Mwisho.