Home SPORTS TIMU YA KIKAPU YA JWTZ YASHIKA NAFASI YA NNE MASHINDANO YA MAJESHI...

TIMU YA KIKAPU YA JWTZ YASHIKA NAFASI YA NNE MASHINDANO YA MAJESHI YA DUNIA UJERUMANI

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Na: Meja Selemani Semunyu.

Timu ya Mpira wa Kikapu kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania iliyokuwa inashiriki Mashindano ya Majeshi ya Dunia imeshika nafasi ya Nne Kati ya Nchi 23 zilizoshiriki Mashindano hayo nchini Ujerumani.

Katika Mchezo  wa Nusu Fainali Tanzania ilipoteza na Ufaransa kwa Vikapu   21 kwa  10 kabla ya kufungwa na Marekani 

Katika kusaka  Mshindi wa Tatu kwa Vikapu  21 kwa 13.

Nafasi ya Kwanza imechukuliwa na Lithuania ikifuatiwa na Ufaransa na nafasi ya Tatu imenyakuliwa na Ufaranssa.

Aidha, Kamati ya ufundi inayoongozwa na Rais wake Luteni Kanali Tom Bellairs imechagua timu ya Tanzania kuwa ni timu  bora na kupewa  kikombe cha Nidhamu ( CISM Fair play Trophy).

Pia Koplo Baraka Sadick amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano ( MVP) huku Meneja  Kapteni Mohamed Kasui na Kocha Sajenti Taji Haleluya Kavalambi wamechaguliwa kuwa wajumbe  wa Kamati ya ufundi.

Timu ya Kikapu ya JWTZ   ilishiriki Mashindano Kama hayo  Mwaka  1993 na kutolewa katika Hatua za Awali.

 Mwisho.