Home LOCAL TANRODS MKOA WA MOROGORO YAANZA KUCHUKUA TAHADHARI.

TANRODS MKOA WA MOROGORO YAANZA KUCHUKUA TAHADHARI.

 

Na: Farida Said,Morogoro.
Wakala wa barabara nchini TANROADS Mkoa wa Morogoro umeanza kuchukua tahadhari kwenye maeneo yote korofi ya barabara na madaraja kwa kukagua uimara wake ili yafanyiwe kazi kabla ya msimu wa mvua kuanza ili kuepusha  maafa na usumbufu kwa watumiaji wa barabara.

Akizungumza katika daraja jipya la Kiyegeya lililopo kata ya Berega wilayani Kilosa katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma, meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Mhandisi Alinanuswe Kyamba alisema ukaguzi huo unalenga kujiweka tayari kwaajili ya kukabiliana majanga ya mafuriko ambayo hutokea wakati  wa msimu wa mvua.
Licha ya ukaguzi huu meneja wa TANRODS Mkoa wa Morogoro alimshukuru  Rais kwa kuiwezesha fedha za kutosha wizara ya ujenzi na uchukuzi kwaajili ya kuimarisha miundombinu ya barabara.

Aidha amewatoa hofu watumiaji wa barabara hiyo kuwa daraja Kiyegea kwa sasa lipo imara na hawategemee mvua yoyete itakayoweza kubomoa miundombinu ya ilipo. 

Msimamizi wa ujenzi wa daraja kiyegea kutoka kampuni ya ujenzi ya CGI Krsto Ilic alisema kabla ya ujenzi wa daraja hilo hali ilikuwa mbaya kwani ilikuwa ni moja ya sehemu hatari zinazosababisha msongamano na ajali za barabarani kutokana na ubovu wa mundombinu yake.

Krsto alisema kuwa daraja lililojengwa pamoja na uimara wake lakini mvua zilizonyesha msimu huu licha kuwa nyingi hazikuweza kuleta madhara katika daraja hilo.

Nao wao baadhi ya wakazi wa eneo la kiyegeya akiwemo bwana Pius Digati wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kukamilisha kwa wakati ujenzi wa daraja hilo kwani tangu kubomoka kwa daraja hilo walikuwa wanapata adha ya usafili kutokana na msongamano.
Daraja la Kiyegeya katika barabara kuu  ya Morogoro- Dodoma  lilobomoka Machi 2, 2020 kutokana na mvua zilizokuwa zimenyesha   mwaka huo   na baadaye kutengenezwa daraja la muda lililowezesha  magari kupita kwa kupokezana kwa zamu.

Katika kuwezesha hatua za awali  ili kurejesha mawasiliano , Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ilinunua makalvati makubwa 120 ya zege kutoka Kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki  inajenga mradi wa Reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam – Makutupora na kujenga daraja la mud ana njia ya mchepuko.

Barabara kuu  hiyo  ni muhimu katika kukuza uchumi  wan chi pamoja nan chi za maziwa makuu zikiwemo za DCR Congo,  Rwanda  na Burundi ambazo bidhaa zake zinapitishwa kwenye  barabara hiyo na inapotokea imekatika  kunachangia kudhorotesha ukuaji wa uchumi  na upatikanaji wa  haraka kubwa za kifedha.
Attachments area

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here