Home BUSINESS SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) LAZINDUA HUDUMA KUBWA YA BIMA FLEX

SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) LAZINDUA HUDUMA KUBWA YA BIMA FLEX

 Mkurugenzi wa Masoko Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Yesaya Mwakifulefule akifafanua jambo wakati akizumngumza katika  uzinduzi wa bidhaa mpya iliyoanzishwa na shirika hilo ijulikanayo kama Bima Flex katika ukumbi wa Julius Nyerere Posta jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa Dkt.Elirehema Dorie akizumngumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya iliyoanzishwa na shirika hilo ijulikanayo kama Bima Flex katika ukumbi wa Julius Nyerere Posta jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa Dkt.Elirehema  Dorie kulia na Mkurugenzi wa Masoko Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Yesaya Mwakifulefule wakiteta jambo wakati wa uzinduzi wa bidhaa ya Bima Flex jijini Dar es salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa Dkt.Elirehema  Dorie kushoto na Mkurugenzi wa Masoko Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Yesaya Mwakifulefule wakipiga makofi mara baada ya uzinduzi rasmi wa bidhaa ya Bima Flex jijini Dar es salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa Dkt.Elirehema  Dorie wa pili kutoka kulia na Mkurugenzi wa Masoko Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Yesaya Mwakifulefule wa pili kutoka kushoto pamoja na wakuu wengine wa vitengo katika shitrika hili wakipiga makofi mara baada ya uzinduzi rasmi wa bidhaa ya Bima Flex jijini Dar es salaam

Picha mbalimbali zikionesha Wakuu wa vitengo mbalimbali pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria katika uzinduzi huo wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi rasmi.

Shirika la Taifa la Bima (NIC) limezindua bidhaa mpya ya Bima kubwa ya Flex ambayo itatoa fursa kwa Taasisi au kikundi kukata Bima hiyo kwa kulipa kidogo kidogo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bima hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Dkt.Elirehema Dorie amesema Bima hiyo inafaida kubwa kwa wenye magari katika Taasisi,Kampuni au kikundi kwa kuzingatia mahitaji yote wakati gari ikiwa imepata ajali.

Amesema Bima ya Flex inatoa nafasi ya kulipa hadi mtu wa tatu katika ajali pamoja na kulipa majeruhi.

Amesema bima hiyo kwa wateja wake wakati gari ikiwa imepata ajali ikiwa matengenezo mteja atalipwa sh.50,000 kwa wiki tatu ambapo gari litakuwa tayari limeshatengenezwa.

Dorie amesema kuwa ulipaji wa Bima hiyo kidogo kidogo hakuna riba watakayotoza lengo ni kuona wateja hawapati usumbufu.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema Shirika limeamua kubadilika kwa kwenda kasi na Mipango ya Serikali kwa baada ya miaka 10 ijayo asilimia 50 watanzania wawe na bima.

Amesema kuwa Shirika litaendelea kutoa elimu ya Bima kwa njia yeyote lengo ni kutaka watanzania wawe na uelewa bima katika kutatua changamoto zao.

Amesema wataendelea kutoa bidhaa mbalimbali za Bima kwa kila eneo kutokana wao wabobezi katika eneo hilo.

Previous articleSHIRIKA LA POSTA LAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA SABASABA
Next articleTANRODS MKOA WA MOROGORO YAANZA KUCHUKUA TAHADHARI.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here