Home BUSINESS SHIRIKA LA POSTA LAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA SABASABA

SHIRIKA LA POSTA LAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA SABASABA


Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo akipokea tuzo ya mtoa huduma bora wa huduma za usafirishaji (Courier and Logistic Exhibitor) kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, mara baada ya kilele cha maonesho hayo jijini Dar es Salaam

Shirika la Posta Tanzania limeibuka kidedea katika tuzo za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), zilizotolewa leo tarehe 13 Julai, 2022, katika viwanja vya Maonesho Sabasaba, jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo zilizoratibiwa na TANTRADE, zimekabidhiwa na Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi katika kilele cha Maonesho hayo tarehe 13 Julai, 2022, jijini Dar es Salaam

Aidha, Shirika la Posta limeibuka kidedea katika kundi la Mtoa huduma bora za Usafirishaji (Courier and Logistic Exhibitor) wa mwaka katika maonesho hayo. Kwa sasa Shirika limeendelea kuboresha miundombinu ya usafirishaji nchini hususani katika kuongeza magari yake na pikipiki kwa ajili ya usambazaji wa mwisho (last mile delivery).

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Postamasta Mkuu,Bwana Macrice Mbodo, ameishukuru Mamlaka hiyo kwa kutambua mchango wa Shirika nchini hasa katika shughuli za Usafirishaji, kwani tuzo hizo zitaendelea kuchochea na kuongeza hamasa kwa Shirika kuendelea kutoa huduka bora kwa wananchi.

Kwa upande wake,naye Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika hilo Bwana Constantine Kasese ameeleza kuwa kwa sasa Shirika la Posta limeendelea kuboresha huduma zake ili kuendena na mahitaji ya sasa ya wananchi.
 
Maonesho haya yaliyokuwa na Kauli Mbiu ya “Tanzania ni sehemu sahihi kwa Biashara na Uwekezaji” yalianza rasmi tarehe 28 Juni, 2022 na yamefungwa leo tarehe 13 Julai, 2022

TANTRADE huwa na utaratibu wa kuandaa tuzo hizi kila mwaka kwa kutambua mchango wa Taasisi/Mashirika/Kampuni katika kutoa huduma kwa wananchi hususani katika kipindi cha maonesho ya Sabasaba.


Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano;
Shirika la Posta Tanzania.
13 Julai, 2022.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here