Mkurugenzi wa Masoko Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Yesaya Mwakifulefule akifafanua jambo wakati akizumngumza katika uzinduzi wa bidhaa mpya iliyoanzishwa na shirika hilo ijulikanayo kama Bima Flex katika ukumbi wa Julius Nyerere Posta jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa Dkt.Elirehema Dorie akizumngumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya iliyoanzishwa na shirika hilo ijulikanayo kama Bima Flex katika ukumbi wa Julius Nyerere Posta jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa Dkt.Elirehema Dorie kulia na Mkurugenzi wa Masoko Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Yesaya Mwakifulefule wakiteta jambo wakati wa uzinduzi wa bidhaa ya Bima Flex jijini Dar es salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa Dkt.Elirehema Dorie kushoto na Mkurugenzi wa Masoko Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Yesaya Mwakifulefule wakipiga makofi mara baada ya uzinduzi rasmi wa bidhaa ya Bima Flex jijini Dar es salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa Dkt.Elirehema Dorie wa pili kutoka kulia na Mkurugenzi wa Masoko Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Yesaya Mwakifulefule wa pili kutoka kushoto pamoja na wakuu wengine wa vitengo katika shitrika hili wakipiga makofi mara baada ya uzinduzi rasmi wa bidhaa ya Bima Flex jijini Dar es salaam
Picha mbalimbali zikionesha Wakuu wa vitengo mbalimbali pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria katika uzinduzi huo wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi rasmi.
Shirika la Taifa la Bima (NIC) limezindua bidhaa mpya ya Bima kubwa ya Flex ambayo itatoa fursa kwa Taasisi au kikundi kukata Bima hiyo kwa kulipa kidogo kidogo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bima hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Dkt.Elirehema Dorie amesema Bima hiyo inafaida kubwa kwa wenye magari katika Taasisi,Kampuni au kikundi kwa kuzingatia mahitaji yote wakati gari ikiwa imepata ajali.
Amesema Bima ya Flex inatoa nafasi ya kulipa hadi mtu wa tatu katika ajali pamoja na kulipa majeruhi.
Amesema bima hiyo kwa wateja wake wakati gari ikiwa imepata ajali ikiwa matengenezo mteja atalipwa sh.50,000 kwa wiki tatu ambapo gari litakuwa tayari limeshatengenezwa.
Dorie amesema kuwa ulipaji wa Bima hiyo kidogo kidogo hakuna riba watakayotoza lengo ni kuona wateja hawapati usumbufu.
Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema Shirika limeamua kubadilika kwa kwenda kasi na Mipango ya Serikali kwa baada ya miaka 10 ijayo asilimia 50 watanzania wawe na bima.
Amesema kuwa Shirika litaendelea kutoa elimu ya Bima kwa njia yeyote lengo ni kutaka watanzania wawe na uelewa bima katika kutatua changamoto zao.
Amesema wataendelea kutoa bidhaa mbalimbali za Bima kwa kila eneo kutokana wao wabobezi katika eneo hilo.