Home BUSINESS NEEC WAENDELEA KUTOA ELIMU KATIKA KLINIKI YA BIASHARA MAONESHO YA SABASABA, SHAKA...

NEEC WAENDELEA KUTOA ELIMU KATIKA KLINIKI YA BIASHARA MAONESHO YA SABASABA, SHAKA AWATEMBELEA

Katibu Mwenezi wa CCM Shaka Habdu Shaka (wa pili kushoto) akizungumza na Afisa Uwezeshaji kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Minaeli Kilimba (kulia) alipofika katika Banda la NEEC lililopo katika Kliniki ya Biashara inayojumuisha Taasisi mbalimbali katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijii Dar es salaam. (wa pili kushoto) ni Mohamed Azizi Afisa Mwanadamizi wa NEEC.

Afisa Mwanadamizi wa NEEC Mohamed Azizi (wa pili kushoto) akifafanua jambo kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Abdu Shaka (wa kwanza kushoto) katika Banda hili kwenye Kliniki ya Biashara iliyopo ndani ya Banda kuu la Wizara ya Viwanda na Biashara katika Maonesho ya Sabsaba Dar es Salaam.
DAR ES SALAAM.
Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) limeendelea kutoa elimu na ushauri kwa wananchi mbalimbali wanaotembelea Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba  namna inavyoteleza majukumu yake na kutatua changamoto zinazowakabili.

NEEC wapo katika Kliniki maalum ya Biashara iliyopo ndani ya Banda la Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ambapo wanatoa elimu kwa wananchi sambamba na kutoa ufumbuzi wa changamoto zao.

Akiongea katika Mahojiano maalum Afisa Mwanadamizi wa NEEC Mohamed Azizi amesema kuwa wananchi wengi wamekuwa na changamoto juu ya uelewa katika eneo zima la uwezeshwaji kiuchumi na mitaji, na kwamba wamekuwa na jukumu kubwa la kuwapa elimu na uelewa kupitia Kliniki hiyo. 

Aidha amesema kuwa pamoja na maeneo mengine pia wanatoa elimu ya kuimarisha mfumo wa elimu ya ujasiriamali na mazingira ya uwekezaji.  

“Tupo hapa Sabasaa kutoa elimu na pamoja na kutoa kutoa majibu sahihi ya maswali ya wananchi, tunapata wageni wengi wanatutembelea pamoja na viongozi na leo tumekuwa na viongozi wengi akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka hbdu Shaka” ameeleza Azizi.




Previous articleDKT. KIRUSWA AKERWA NA WANAOKIUKA SHERIA YA MADINI
Next article“GESI ASILIA TULIYOIGUNDUA ITAKUWA NA SOKO KUBWA NDANI YA MIAKA 30 ” MHANDISI SANGWENI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here