Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 23, 2022 amefanya ziara ya siku moja katika mkoa wa Arusha na Tanga ambapo atashuhudia zoezi la awamu ya pili la wananchi wapatao 117 kutoka kaya 27 wanaohama kwa hiari yao wenyewe kutoka katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro kuelakea kijiji cha Msomera, Handeni.

.jpeg)
.jpeg)
Pia Mheshimiwa Majaliwa atakagua Makazi na miundombinu iliyopo katika makazi mapya watakayohamia wananchi hao zikiwemo huduma za kijamii katika kijiji cha Msomera, Handeni mkoani Tanga.