Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) akisisitiza jambo mbele ya Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Chen Mingjian wakati wawili hao walipokutana kwa mazungumzo yanayolenga kujenga uwezo wa ukuzaji TEHAMA nchini; Mkutano huo ulifanyika Jumatano tarehe 15 Juni, 2022 jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) akiagana na mgeni wake Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Chen Mingjian muda mfupi baada ya kuhitimisha mazungumzo yaliyolenga kujenga uwezo wa ukuzaji TEHAMA nchini; mkutano huo ulifanyika Jumatano tarehe 15 Juni, 2022 jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) akipokea utambulisho wa wasaidizi wa Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Chen Mingjian wakati alipokutana nae kwa mazungumzo. Mazungumzo yalilenga kutazama maeneo ya ushirikiano ili kujenga uwezo wa ukuzaji TEHAMA nchini; mkutano huo ulifanyika Jumatano tarehe 15 Juni, 2022 jijini Dar es salaam. Picha: TCRA.