NA: JEREMIA ERNEST
BARAZA la sanaa Basata lime wapongeza wandaaji na wadhamini wa shindano la Miss Tanzania 2022 kwa kukamilisha mchakato wa mchuano huo kwa viwango vya juu.
Shindano la Miss Tanzania lilifanyika Mai 20 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar Es Salaam, ambapo Halima Ahmad Kopwe, aliibuka mshindi na kukabidhiwa gari yenye thamani ya milioni 40 na fedha milion 10 kwa ajili ya maandalizi ya shindano la dunia.
Akizungumaza na wandishi wa habari kaimu Katibu mkuu wa Baraza la Sanaa Matiko Mniko, amesema wamefurahishwa na uendeshaji wa shindano hilo.
“Kwa niaba ya serekali niwapongeze wandaaji wa shindano hili The Look Campan Limited, pamoja na wadhamini Star Times, kwa kuandaa shindano lenye kiwango cha juu na kutoa zawadi zenye thamani ya kuheshimisha tasnia ya urembo hapa nchini sisi kama Baraza la Sanaa tuna watunuku vyeti vya pongezi na baruau,” anasema Matiko Mniko.
Naye mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Azama Mashango, amesema wanafurahi kwa kuwa Basata wame tambua kazi yao na kuomba waendelee kuwashika mkono ili kukuza tasnia ya urembo.
Kwa upande wa wandaaji Afisa Masoko wa Star Times David Malisa amesema tayari wameanza kujiandaa kwa msimu mpya wa shindano hilo kwa sababu wanataka kufanya vizuri zaidi.
“Tunashukuru kwa pongezi za Basata tumezipokea na tuna ahidi kuboresha zaidi shindano hilo tumejipanga kwa msimu ujao tutaanzia ngazi ya mkoa, kanda mpaka Taifa ili kuboresha zaidi.”