Home SPORTS YANGA YATANGAZA MSHAMBULIAJI MPYA

YANGA YATANGAZA MSHAMBULIAJI MPYA

MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga SC wamemtambulisha mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia, Lazarous Kambole kuwa mchezaji wake mpya wa kwanza kuelekea msimu ujao.

Kambole mwenye umri wa miaka 28, anatua Jangwani akitokea Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini aliyojiunga nayo mwaka 2019 akitokea ZESCO United ya kwao.

Kambole aliibukia Konkola Mine Police mwaka 2011, kabla ya kuhamia Konkola Blades mwaka 2013 ambako alicheza hadi 2014 alipokwenda ZESCO United – na tangu mwaka 2018 amekuwa akichezea timu ya taifa, Chipolopolo

Previous articleUANDISHI WA HABARI NA CHANGAMOTO ZA KIDIGITI
Next articleSTAR TIMES, THE LOOK WAPEWA PONGEZI BASATA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here