Home KIDSNEWS SERIKALI YATAKA USHIRIKIANO WA WADAU KATIKA KUPINGA UKATILI WA UTUMIKISHWAJI WA KAZI...

SERIKALI YATAKA USHIRIKIANO WA WADAU KATIKA KUPINGA UKATILI WA UTUMIKISHWAJI WA KAZI KWA WATOTO


Kijana kutoka shirika la Mtoto Wetu Tanzania Elizabeth Philipo akielezea changamoto alizopitia kabla ya kupata msaada katika shirika hilo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupingwa Utumikishwaji wa Watoto yaliyofanyika katika ukumbi wa Royal Village Hotel Jijini Dodoma Juni 12, 2022.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akizungumza na vijana na watoto katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupingwa Utumikishwaji wa Watoto yaliyofanyika katika ukumbi wa Royal Village Hotel Jijini Dodoma Juni 12, 2022. Kaulimbiu ikisemwa: Utumikishwaji wa Watoto ni Kikwazo cha Maendeleo Endelevu Wadau Tushikamane Kutokomeza.


 
Sehemu ya Watoto walio hudhuria Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupingwa Utumikishwaji wa Watoto yaliyofanyika katika ukumbi wa Royal Village Hotel Jijini Dodoma Juni 12, 2022.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajiara na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (katikati) akichangia jambo wakati wa mdahalo uliofanyika kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupingwa Utumikishwaji wa Watoto, (kulia) ni Afisa Elimu Kazi Mwandamizi na Mwakilishi wa Kamisha wa Kazi (OWM-KVAU) Honesta Ngolly na (kushoto) ni Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Kupinga Utumikishwaji wa Watoto Tanzania Scholastica Pembe.

 

PICHA ZOTE NA 

OFISI YA WAZIRI MKUUKAZI, VIJANA , AJIRA, NA WENYE ULEMAVU.

 

Serikali imetaka ushirikiano na wadau wa kupinga utumikishwaji wa kazi kwa watoto ili kufanikiwa kukomesha utumikishwaji huo  hapa nchini.

Wadau ambao hawanabudi kutoa ushirikiano madhubuti kwa Serikali ni pamoja na Mashirika ya Kimataifa, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Vyama vya Wafanyakazi, Vyama vya Waajri, Asasi za Kidini na za Kiraia pamoja na  wananchi.

Hayo ameyasema Leo,  jijini Dodoma Juni 12, 2022,  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Mhe. Patrobasi Katambi,  wakati  wa kuadhimisha siku ya Kupinga Utumikishwaji wa kazi kwa watoto Duniani.

Kauli mbiu ya Maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni:
“Utumikishwaji wa Watoto ni Kikwazo cha Maendeleo Endelevu, Wadau Tushikamane Kuutokomeza”

Mhe. Katambi, amesisitiza  kila mdau  kuhakikisha haki za msingi za watoto zinalindwa kwa kutimiza wajibu wake.

“Katika kutokomeza Utumikishwaji wa Watoto katika kazi hatarishi lazima  mzingatie matakwa  ya  Mikataba ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) na mapendekezo yake kupitia Sheria za Kazi za hapa nchini”

Mhe.Katambi ameongeza kuwa, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Serikali (Integrated Labour Force Survey) wa mwaka 2014, umeonesha,  29% ya watoto wenye umri kati ya miaka 5- 17 sawa na watoto millioni 4.2, wavulana wakiwa ni  29.3% na wasichana  28.4% wako katika utumikishwaji .

Aidha, amefafanua kuwa utafiti huo umebainisha kuwa,  watoto wengi wapo  katika sekta  za kiuchumi ikiwa ni pamoja na mashambani, majumbani, migodini, na biashara ndogondogo.

Kwa mujibu wa utafiti huo, sababu kuu zinazo chochea matukio ya utumikishwaji  ni Umasikini, Vifo vya Wazazi na Walezi, Mifarakano katika Familia, Mila na Desturi zisizofaa pamoja na Nguvu Kazi Rahisi (Cheap Labour).

Pia, unabainisha madhara ya moja kwa moja  yanayosababishwa na utumikishaji wa watoto ni Kuwa na Taifa la Watu Wasiojua Kusoma na Kuandika pamoja na Kuenea kwa Magonjwa  kama vile UKIMWI.

Kwa  mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Mtoto ametafsiriwa kuwa ni mtu yeyote mwenye Umri wa chini ya miaka 18.

Previous articleCHAMA CHA USHIRIKA CHA MUUNGANO KIZIGUZIGU KAKONKO KIGOMA KUUZA TANI 400 ZA MAHARAGE WFP
Next articleRAIS SAMIA AZUNGUMZA NA VIONGOZI WANAWAKE AMBAO NI WAKUU WA TAASISI MBALIMBALI NCHNI OMAN
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here