Home BUSINESS SERIKALI KUTATUA MGOGORO KIWANDA CHA KATANI JIJINI DAR

SERIKALI KUTATUA MGOGORO KIWANDA CHA KATANI JIJINI DAR

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji (wa kwanza kushoto mwenye nguo nyekundu) akiwasili katika kiwanda cha kuchakata Mkonge cha 21st Century Textiles Limited alipofanya ziara kwenye kiwanda hicho leo Juni 17,2022 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha kuchakata mkonge cha 21st Century Holdings LTD leo Juni 17,2022 Jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi wa kiwanda cha kuchakata Mkonge cha 21st Century Holdings LTD wakipiga makofi kumpongeza Waziri Kijaji kwakuzungumza nao na kuwapatia majawabu wa maswali yao pamoja na kuwahakikishia ajira yao Kiwandanihapo.
Mmoja wa Mfanyakazi wa Kiwanda hicho akitoa maelezo kwa Mhe. Waziri Dkt. Kijaji (hayumo pichani) juu ya mustakabali wa maisha yao kutokana na mgogoro uliopo Kiwandani hapo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji akitoka katika Ofisi za kiwanda hicho mara baada ya kufanya ziara na kuzungumza na uongozi wa kiwanda hicho leo Juni 17,2022 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kiwanda cha kuchakata Mkonge cha 21st Century Holdings LTD alipofanya ziara kwenye kiwanda hicho leo Juni 17,2022 Jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO).
 
Tazama Video.

https://youtu.be/wtjN6SmRFaI

Na: HUGHES DUGILO, DAR ES SALAAM.

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa Serikali imejipanga kuchukua hatua madhubuti za kutatua changamoto zote zinazoikabili sekta ya viwanda nchini hususani vile vinavyochakata na kuzalisha bidhaa za katani ili viweze kufanya shughuli zake katika mifumo sahihi iliyowekwa na serikali.

Kauli hiyo ameitoa leo Juni 17,2022 Jijini Dar es Salaam alipozungumza 21st Century Holdings LTD kinachojihusisha na uchakataji wa  kamba zinazotokana na mkonge kilichopo chang’ombe kilichopo Jijini humo.

Akiongea na wafanyakazi hao Dkt. Kijaji amesema katika kutatua changamoto hizo Serikali imeondoa kodi ya ongezeko la thamani kwenye mazao yote yanayotokana na zao Mkonge  ikiwa ni lalamiko lao kubwa la wenye viwanda vinavyozalisha bidhaa za katani.

Pia Amesema Serikali inaendelea kushughulikia changamoto nyingine ili kuviwezesha viwanda hivyo kushiriki kikamilifu katika soko la ushindani ndani ya nchi, kikanda na kimataifa.

Aidha, Dkt. Kijaji amewahakikishia wafanyakazi wa kiwanda hicho kuwa  kiwanda hicho hakitafungwa kwa kuwa Serikali inashughulikia changamoto zinazokikabili kiwanda hicho pamoja na zinazowakabili wafanyakazi hao  ikiwemo upatikanaji wa maslahi na haki zao za msingi.

Amesema katika kuhakikisha viwanda hivyo vinakuwa na mazingira wezeshi imeondoa kodi ya ongezeko la thamani kwenye mazao ya Mkonge ambalo ndio malighafi kuu katika viwanda hivyo. 

“Katika Mwaka wa fedha ujao Serikali inatarajia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Sekta ya Viwanda ili kila muhusika wa eneo hilo anufaike hatimaye kuongeza ajira na uchumi kwa ujumla hapa nchini”. Amesema Dkt. Kijaji.

Aidha Waziri huyo amezungumzia uwepo wa ushindani wa Bidhaa nyingine ya mazao ya nyuzi za lailoni  na kwamba wizara yake inaendelea kulifanyia kazi na kulipatia ufumbuzi suala hilo ili kuliondoa tatizo hilo ambalo linasababisha viwanda hivyo kutofanya kazi zake inayopaswa.
 
“kuweni na amani Serikali tuko hapa tumekuja tuongee kwa pamoja na wenye kiwanda ili tuone changamoto wanazokutana nazo na tuweze  kuzishughulikia na nyinyi watanzania muweze kuendelea na ajira zenu” ameongeza Waziri Kijaji.
 
Na kuongeza kuwa “Hakuna anayekwenda kupoteza kazi, na kama ikitokea utapoteza kazi hupotezi haki yako, nchi hii inaongozwa kwa sheria lazima taratibu zote zifuatwe endepo mtu ataondoka katika nafasi yake” ameongeza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here